Ambao uwapatapo msiba husema: Hakika, sisi ni wa Allah, na kwake yeye tu tutarejea
Tazama kadi
Na lau tungelifanya Qur’ani kwa lugha ya kigeni wangelisema: Kwanini Aya zake hazikupambanuliwa? Yawaje lugha ya kigeni na Mtume Mwaarabu? Sema: Hii Qur’ani ni uongofu na ponyo kwa wenye kuamini. Na wasio amini umo uziwi katika masikio yao, nayo kwao imezibwa hawaioni. Hao wanaitwa nao wako pahala pa mbali
Kujisahau kunasababisha nyoyo kuwa ngumu. Na kumkumbuka Allah kunazilainisha nyoyo na kuzihuisha upya. Usisubiri kufunikwa na dunia, bali rudi hivi sasa kwa Allah na umuabudu Yeye tu! MAZINGATIO: Ni wajibu kurejea kwa Allah kwa kumkumbuka.
Qur’an husomwa ili kuzifundisha nyoyo maadili mema. Na Sala husimamishwa ili kuzisafisha nafsi ziwe na tabia njema. Basi, mwenye kudumisha mafungamano yake na Mola wake Mlezi, atapata ulinzi wake wa kutokuwa na maadili mabaya. MAZINGATIO: Athari ya Sala katika maisha ya mtu na jamii
Hakuna katika dunia kitu kikubwa sana kuliko kumkumbuka Allah. Ni nuru ya nyoyo, na kinga ya nafsi, na ngazi ya kuthibiti katika haki. Kila unapomkumbuka na kumtaja Allah kwa dhati ya ukweli kabisa, basi utakuwa karibu yake sana! MAZINGATIO: Kumkumbuka Allah ni jambo kubwa sana.
Enyi mlioamini, ombeni msaada kwa uvumilivu (subra) na kuswali. Bila shaka, Allah yupo pamoja na wenye uvumilivu
Allah hamtelekezi mwenye kusubiri, bali huwa pamoja naye katika dhiki zake na masikitiko yake yanayomtoa machozi, na katika kila sijda anayo ifanya mja mwema huwa kuna matarajio makubwa ya msaada wa Allah. MAZINGATIO: Allah yu pamoja na wanao subiri