Ambao uwapatapo msiba husema: Hakika, sisi ni wa Allah, na kwake yeye tu tutarejea
Tazama kadi
Kujaribiwa si ishara ya kuchukiwa na Allah, bali ni fursa ya kupanda daraja la juu kwa wenye subira. Khofu, njaa, na upungufu wa vitu mbali mbali, vyote hivyo ni masomo muhimu katika kumuamini Allah Mtukufu. MAZINGATIO: Ni wajibu kujifunza katika majaribio na kuwa na subira
(Allah) Mwingi wa rehmaAmefundisha Qur’aniAmemumba mwanadamuAmemfundisha kusema (yaliyomo moyoni)
Je! Hawaizingatii hii Qur’ani? Au kwenye nyoyo (zao) zipo kufuli?
Unaweza kufikiwa na hali ya dhiki, na ikakukosesha katika dunia hii sehemu ya mali yako na roho za uwapendao. Lakini, mwenye kusubiri na kuridhia qadar ya Allah kwa majaribio hayo, basi hupata bishara njema ya kufanikiwa kutoka kwa Mola wake Mlezi! MAZINGATIO: Subira ni nuru katika maisha
Moyo uliyo fungwa kwa matamanio hauwezi kufikiwa na nuru ya Qur’an. Na ufunguo wake ni: kuzingatia, kunyenyekea, na kuwa mkweli wa kuitafuta haki. MAZINGATIO: Ufungue moyo wako kwa Qur’an.
Katika vipindi vya misiba, haitakiwi kusema sema maneno ya upuuzi! bali inatosha tu kuzingatia kwa Yakini na kurejea maneno mazuri kwa kusema: “Sisi ni wa Allah, na kwake Yeye tutarejea” ndani ya maneno hayo ndiyo ishara ya kujisalimisha kwa Allah na kuridhia qadar yake na kupata utulivu wa nafsi. MAZINGATIO: Umuhimu wa kujisalimisha na kurejea k...