(Allah) Mwingi wa rehma
Amefundisha Qur’ani
Amemumba mwanadamu
Amemfundisha kusema (yaliyomo moyoni)
Tazama kadi
Qur’an haikuteremshwa kwa ajili ya mapambo wala kupata baraka tu, bali imeteremshwa ili tuifahamu na kuizingatia, na kufuata muongozo wake katika kila jambo. MAZINGATIO: Ni wajibu kuizingatia Qur’an Tukufu
Nyoyo ndiyo zinazo fahamu, siyo masikio. Basi, yeyote mwenye kuufungua moyo wake kwa kuifuata haki, atapata katika Qur’an nuru. Na mwenye kuufunga moyo wake, basi hautosikia chochote, hata kama atasomewa Aya zote. MAZINGATIO: Nyoyo ndiyo husikia na kuzingatia.
Qur’an imekuwa ni neema ya kwanza baada ya rehema za Allah. Na inatufunza kuwa neema kubwa aliyo fundishwa mwanaadam baada ya kuumbwa kwake ni kupewa ujuzi wa maneno ya Allah (Qur’an). MAZINGATIO: Qur’an ni rehema.
Soma uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Sala. Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumtaja Allah ndilo jambo kubwa kabisa. Na Allah anayajua mnayo yatenda
Hakuna katika dunia kitu kikubwa sana kuliko kumkumbuka Allah. Ni nuru ya nyoyo, na kinga ya nafsi, na ngazi ya kuthibiti katika haki. Kila unapomkumbuka na kumtaja Allah kwa dhati ya ukweli kabisa, basi utakuwa karibu yake sana! MAZINGATIO: Kumkumbuka Allah ni jambo kubwa sana.
Unaweza kufikiwa na hali ya dhiki, na ikakukosesha katika dunia hii sehemu ya mali yako na roho za uwapendao. Lakini, mwenye kusubiri na kuridhia qadar ya Allah kwa majaribio hayo, basi hupata bishara njema ya kufanikiwa kutoka kwa Mola wake Mlezi! MAZINGATIO: Subira ni nuru katika maisha