(Allah) Mwingi wa rehma
Amefundisha Qur’ani
Amemumba mwanadamu
Amemfundisha kusema (yaliyomo moyoni)
Tazama kadi
Hakuna katika dunia kitu kikubwa sana kuliko kumkumbuka Allah. Ni nuru ya nyoyo, na kinga ya nafsi, na ngazi ya kuthibiti katika haki. Kila unapomkumbuka na kumtaja Allah kwa dhati ya ukweli kabisa, basi utakuwa karibu yake sana! MAZINGATIO: Kumkumbuka Allah ni jambo kubwa sana.
Je! ni nyoyo ngapi zilizo jiweka mbali na kumkumbuka Allah, mpaka zikawa ngumu na kususuwaa, hali ya kuwa bado wito wa Allah, Mola Mlezi wa viumbe unawaita na kuzitaka zirudi katika unyenyekevu. Je! haujafika wakati kwa nyoyo hizo kunyenyekea? MAZINGATIO: Umuhimu wa kuzizindua nyoyo kutokana na kujisahau, katika kumkumbuka Allah
Kila Aya katika Qur’an imebeba ujumbe maalumu. Na kila mwenye kuitumia akili yake na moyo wake katika kuizingatia Qur’an basi atapata nuru na elimu ya ufahamu wa mambo. MAZINGATIO: Nuru ya Qur’an inaangaza daima
Wakati unapo fikwa na majanga, usitafute ufumbuzi wa nje kwanza. Bali rudi kwenye Subira na Sala, ndani yake kuna msaada mkubwa wa kutoka mbinguni kwa Allah. MAZINGATIO: Umuhimu wa kushikamana na Subira na Sala
Qur’an siyo Kitabu kinacho somwa tu. Bali ni Kitabu cha kuzingatiwa! Yeyote asiye zingatia maana yake, ana kuwa kama mtu ambaye moyoni mwake kuna kufuli lisilo funguka! MAZINGATIO: Ni wajibu kuizingatia Qur’an Tukufu
Qur’an ina kuongoa kwenye njia iliyo nyooka. Si kwa maamrisho tu na makatazo, bali ni muongozo wa maisha yako yote kwa kukupa mafanikio na utukufu. MAZINGATIO: Qur’an ni muongozo wa maisha.