Maisha haya ya duniani ni mafupi sana vyovyote vile yatakavyo refuka. Na lengo kuu si kupata mapambo ya dunia, bali ni kupata mafikio mazuri ambayo haya kimbiliki.
Enyi watu! Hakika ahadi ya Allah ni ya kweli. Basi yasiku-danganyeni maisha ya dunia, wala mdanganyifu asikudanganyeni juu ya Allah
Hakika Shetani ni adui yenu, basi mfanyeni kuwa ni adui. Kwani yeye analiita kundi lake liwe katika watu wa Motoni
FAATWIR
(5-6)

Kumbuka kuwa udanganyifu mkubwa upo katika kushughulishwa na vitu vya muda mfupi na kujisahau kushughulishwa na vitu vya kudum milele!
MAZINGATIO:
Ni wajibu kuchukua mazingatio katika kujiandaa na maisha ya akhera.
Enyi watu! Hakika ahadi ya Allah ni ya kweli. Basi yasiku-danganyeni maisha ya dunia, wala mdanganyifu asikudanganyeni juu ya Allah
Hakika Shetani ni adui yenu, basi mfanyeni kuwa ni adui. Kwani yeye analiita kundi lake liwe katika watu wa Motoni
FAATWIR
(5-6)
Adui mkubwa si yule anaye gombana nawe duniani, bali ni yule anaye taka kukupotosha katika njia ya Allah.
Kulizingatia jambo hili muhimu kutabadilisha vipaumbele vyako, na kuulinda moyo wako kutojisahau kufanya yale yenye manufaa nawe katika maisha ya milele.
Hakika, wamepata hasara wale waliopinga kukutana na Allah, hadi kitakapowajia Kiyama ghafla watasema: Eee! Majuto ni yetu kwa (sababu ya) yale tuliyoyafanyia uzembe humo (duniani), na huku wanabeba mizigo (makosa) yao migongoni mwao. Elewa kwamba, ni mabaya mno hayo (madhambi) wanayoyabeba
Na maisha ya duniani si chochote isipokuwa tu ni mchezo na pumbao. Na kwa yakini kabisa, nyumba ya Akhera ndio bora zaidi kwa wanaomcha Allah. Je, hamtumii akili?
AL AN’ĀM
(31-32)
Hasara kubwa ni umri kupita katika kujisahau. Kisha mtu kuzinduka katika wakati ulio kwisha!
Majuto katika siku ya kiama hayatofaa, basi anza leo kufanya yale yatakayo kuokoa kesho!
MAZINGATIO:
Ni muhimu kuwa na mazingatio ya kujiandaa na nyumba ya akhera.
Hakika, wamepata hasara wale waliopinga kukutana na Allah, hadi kitakapowajia Kiyama ghafla watasema: Eee! Majuto ni yetu kwa (sababu ya) yale tuliyoyafanyia uzembe humo (duniani), na huku wanabeba mizigo (makosa) yao migongoni mwao. Elewa kwamba, ni mabaya mno hayo (madhambi) wanayoyabeba
Na maisha ya duniani si chochote isipokuwa tu ni mchezo na pumbao. Na kwa yakini kabisa, nyumba ya Akhera ndio bora zaidi kwa wanaomcha Allah. Je, hamtumii akili?
AL AN’ĀM
(31-32)
Dunia kwa hali yoyote itakavyo kudanganya, bado itabakia tu kuwa ni upuuzi na mchezo.
Ama utukufu wenye kubaki, ni kwa yule atakaye ishi kwa uchamungu, anaye jua kuwa njia ya kumtii Allah ndio chumo bora la kushikamana nalo.
MAZINGATIO:
Njia ya kuokoka ipo katika kuzinduka kwa roho katika kufanya mema.
Jueni kwamba maisha ya dunia ni mchezo na pumbao na mapambo, na kufakharishana baina yenu na kushindana kwa wingi wa mali na watoto; ni kama mfano wa mvua inayowafurahisha wakulima mimea yake, kisha yananyweya, kisha utayaona yamepiga manjano, kisha yanakuwa mabua. Na Akhera kuna adhabu kali, na msamaha kutoka kwa Allah na radhi zake. Na uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni sterehe fupi za udanganyifu
AL-HADIID
(20)
Mapambo ya dunia yana fanana na mmea ambao unavutia machoni kwa muda, kisha unakauka haraka.
Usiufanye umri wako kuangamia kwa vitu vyenye kupita, bali tafuta yatakayo baki nawe baada ya kuondoka katika haya maisha ya dunia.
MAZINGATIO:
Tuchukue mazingatio katika haya maisha yanayo ondoka.
Jueni kwamba maisha ya dunia ni mchezo na pumbao na mapambo, na kufakharishana baina yenu na kushindana kwa wingi wa mali na watoto; ni kama mfano wa mvua inayowafurahisha wakulima mimea yake, kisha yananyweya, kisha utayaona yamepiga manjano, kisha yanakuwa mabua. Na Akhera kuna adhabu kali, na msamaha kutoka kwa Allah na radhi zake. Na uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni sterehe fupi za udanganyifu
AL-HADIID
(20)
Mwanaadam yupo katika kuchagua njia mbili: njia ya starehe ya muda inayo upumbaza moyo au msamaha na radhi za Allah zisizo isha.
Enyi watu tumewaumbeni wanaume na wanawake na tumewafanyeni mataifa na makabila ili mutambuane hakika mbora zaidi wenu kwa Allah ni zi mno mwenye mcha Mungu zaidi kwenu hakika Allah ni mjuhabari nyingi
AL-HUJURAAT
13
Kutofautiana watu kwa rangi na nasabu sio sababu ya kuzidiana au kutengana. Bali ni njia tu ya kujuana na ukamilifu.
Kipimo cha kweli cha utukufu ni usafi wa moyo na uchamungu tu.
Enyi watu tumewaumbeni wanaume na wanawake na tumewafanyeni mataifa na makabila ili mutambuane hakika mbora zaidi wenu kwa Allah ni zi mno mwenye mcha Mungu zaidi kwenu hakika Allah ni mjuhabari nyingi
AL-HUJURAAT
13
Mwanaadam hatukuzwi kwa ukoo wake, wala mali wala muonekano wake, bali utukufu wake upo katika ukweli wake katika kumtii Allah na uchamungu.
MAZINGATIO:
Utukufu wa kweli katika uchamungu ndiyo njia ya wokovu..
Hayo ndiyo makazi ya Akhera, tumewafanyia wale wasio taka kujitukuza duniani wala ufisadi. Na mwisho mwema ni wa wacha Mungu
Atakaye tenda wema atapata malipo bora kuliko huo wema alioutenda. Na atakaye tenda uovu, hawalipwi watendao uovu ila waliyokuwa wakiyatenda
AL-QASWAS
(83-84)
Maisha ya milele si kwa wale wenye kiburi na ufisadi, bali ni kwa yule mwenye unyenyekevu wa moyo wake na kumcha Mola wake Mlezi.
Hayo ndiyo makazi ya Akhera, tumewafanyia wale wasio taka kujitukuza duniani wala ufisadi. Na mwisho mwema ni wa wacha Mungu
Atakaye tenda wema atapata malipo bora kuliko huo wema alioutenda. Na atakaye tenda uovu, hawalipwi watendao uovu ila waliyokuwa wakiyatenda
AL-QASWAS
(83-84)
Mizani ya akhera ni adilifu: jema moja humuongoza mtu kwenye malipo makubwa, na kwa ovu hatolipwa mwenye nalo ila kwa vile alivyo fanya.
Fursa ya leo(duniani) ni kuwa makini katika kuchagua yale mambo ya kubeba yatakayo kunufaisha kesho(akhera).
Na msiwaoe wale walio olewa na baba zenu ispokuwa yaliyopita, tendo hilo ni baya na bughdha na ni njia mbaya
Wameharamishwa kwenu mama zenu, na binti zenu na dada zenu na shangazi zenu, na ndugu wa mama zenu na watoto wa kaka zenu, na watoto wa dada zenu, na mama zenu ambao wamewanyonyesha na dada zenu wa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wa wake zenu ambao wapo majumbani mwenu wanaotokana na wake mlio waingilia, kama (wake hao) hamjawaingilia, basi sivibaya kwenu[1]. Na (ni haramu kwenu) wake wa watoto wenu wa kuwazaa na (ni haramu) kuwakusanya mtu na dada yake ispokua yale yaliyopita, hakika Allah ni mwenye kusamehe mpole mno
ANNISAI
(22-23)
Uislamu haukuacha mahusiano yaende bila vidhibiti, bali umeweka mifumo inayo linda familia zisiharibiwe, na kulinda vizazi na utu wa kibinaadam.
Na msiwaoe wale walio olewa na baba zenu ispokuwa yaliyopita, tendo hilo ni baya na bughdha na ni njia mbaya
Wameharamishwa kwenu mama zenu, na binti zenu na dada zenu na shangazi zenu, na ndugu wa mama zenu na watoto wa kaka zenu, na watoto wa dada zenu, na mama zenu ambao wamewanyonyesha na dada zenu wa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wa wake zenu ambao wapo majumbani mwenu wanaotokana na wake mlio waingilia, kama (wake hao) hamjawaingilia, basi sivibaya kwenu[1]. Na (ni haramu kwenu) wake wa watoto wenu wa kuwazaa na (ni haramu) kuwakusanya mtu na dada yake ispokua yale yaliyopita, hakika Allah ni mwenye kusamehe mpole mno
ANNISAI
(22-23)
Walioharamishwa na Allah kuwaoa si kwa lengo baya, bali ni kwa ajili ya kulinda heshima na rehema kwa jamii, ili mafungamano yabakie safi na familia kuwa na utulivu na jamii kuwa na amani.
Na (ni haramu kwenu) wanawake walio katika ndoa isipokuwa wale mliowamiliki kwa mikono yenu ya kuume[1], (hili) Allah ameandika kwenu, na mmehalalishiwa (wanawake) wasiokuwa hawa mtake kwa mali zenu, kujilinda na kutofanya zinaa. Na wale (wake) mliokaa nao faragha (baada ya ndoa) kati ya hao, wapeni mahari yao ni lazima. Na si vibaya kwenu kwa mliyoridhiana katika yale yaliyotajwa[2]baada ya kutimiza wajibu, hakika Allah ni mjuzi mwenye hekima
24 ANNISAI
Ndoa katika Uislamu imesimama juu ya misingi ya usafi na heshima, na si juu ya misingi ya upuuzi na matamanio holela.
Ni mkataba wa kimajukumu unao linda heshima na kutimiza haki.
MAZINGATIO:
Ndoa ni jukumu la kusimamia haki na utekelezaji wa thamani ya uislamu.
Na (ni haramu kwenu) wanawake walio katika ndoa isipokuwa wale mliowamiliki kwa mikono yenu ya kuume[1], (hili) Allah ameandika kwenu, na mmehalalishiwa (wanawake) wasiokuwa hawa mtake kwa mali zenu, kujilinda na kutofanya zinaa. Na wale (wake) mliokaa nao faragha (baada ya ndoa) kati ya hao, wapeni mahari yao ni lazima. Na si vibaya kwenu kwa mliyoridhiana katika yale yaliyotajwa[2]baada ya kutimiza wajibu, hakika Allah ni mjuzi mwenye hekima
24 ANNISAI
Mahusiano katika uislamu hujengwa juu ya misingi ya ridhaa na uadilifu, si kwa mabavu na fujo.
Yale yote yaliyo faradhishwa katika ndoa ni dhamana ya kulinda haki za mwanamke na kuleta utulivu wa familia.
Enyi mlio amini! Msiingie nyumba zisizo nyumba zenu mpaka mwombe ruhusa, na mwatolee salamu wenyewe. Hayo ni bora kwenu ili mpate kukumbuka
Na msipo mkuta mtu humo basi msiingie mpaka mruhusiwe. Na mkiambiwa: Rudini! Basi rudini. Hivi ni usafi zaidi kwenu. Na Allah anajua mnayo yatenda
ANNUUR
27-28
Nyumba si kuta tu, bali ni mjumuiko wa uwanda wa amani na utulivu wa watu wake.
Kwa ajili hiyo, Uisalmu umeweka utaratibu wa kuomba idhini ya kuingia katika majumba kwa ajili ya usalama na kulinda haki maalumu za wakazi na kuleta heshima.
MAZINGATIO:
Adabu za kuomba idhini ni katika mambo matukufu ya Uislamu
Enyi mlio amini! Msiingie nyumba zisizo nyumba zenu mpaka mwombe ruhusa, na mwatolee salamu wenyewe. Hayo ni bora kwenu ili mpate kukumbuka
Na msipo mkuta mtu humo basi msiingie mpaka mruhusiwe. Na mkiambiwa: Rudini! Basi rudini. Hivi ni usafi zaidi kwenu. Na Allah anajua mnayo yatenda
ANNUUR
27-28
Kubisha hodi kwa adabu, na kuondoka usipo ruhusiwa kuingia kwa mtu si udhaifu, bali ni usafi wa nafsi, na jamii kubakia kuishi katika misingi ya aibu na heshima.
MAZINGATIO:
Kushikamana na tabia za kiislamu ni njia ya wokovu.
Enyi mlio amini! Nawakutakeni idhini iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia na walio bado kubaleghe miongoni mwenu mara tatu - kabla ya Sala ya alfajiri, na wakati mnapo vua nguo zenu adhuhuri, na baada ya Sala ya ishaa. Hizi ni nyakati tatu za faragha kwenu. Si vibaya kwenu wala kwao baada ya nyakati hizi, kuzungukiana nyinyi kwa nyinyi. Hivyo ndivyo Allah anavyo kuelezeni Aya zake, na Allah ni Mjuzi Mwenye hekima
ANNUUR
58
Uislamu umetufundisha kuwa nyumba zina nyakati maalumu za kuingia ndani yake,
Hata Watoto ina takiwa walelewe katika kuziheshimu.
Kumfundisha adabu mtoto ni moja wapo ya kujenga jamii safi, inayo linda aibu na sitara.
Enyi mlio amini! Nawakutakeni idhini iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia na walio bado kubaleghe miongoni mwenu mara tatu - kabla ya Sala ya alfajiri, na wakati mnapo vua nguo zenu adhuhuri, na baada ya Sala ya ishaa. Hizi ni nyakati tatu za faragha kwenu. Si vibaya kwenu wala kwao baada ya nyakati hizi, kuzungukiana nyinyi kwa nyinyi. Hivyo ndivyo Allah anavyo kuelezeni Aya zake, na Allah ni Mjuzi Mwenye hekima
ANNUUR
58
Nidhau ya kuomba idhini ya kuingia majumbani katika nyakati za kupumzika, si unyanyasaji wa kijinsia. Bali ni mafundisho ya Allah yanayo linda familia na kuzilea katika hali ya usafi na heshima ya kudumu.
MAZINGATIO:
Kushikamana na tabia za kiislamu ni njia ya wokovu.
Na watoto wanapo fikia umri wa kubaleghe basi nawatake ruhusa, kama walivyo taka ruhusa wa kabla yao. Hivyo ndivyo anavyo kubainishieni Allah Aya zake, na Allah ni Mjuzi Mwenye hekima
ANNUUR
59
Kuwalea Watoto katika maadili ya kuomba idhini ya kuingia majumbani tangu utotoni mpaka kubaleghe kwao kunaleta kuwa na tabia ya kuona aibu daima, na kuzilinda nyumba kutokana na fujo, na kujaalia heshima kutawala katika nafsi.
MAZINGATIO:
Malezi ya kiislamu ni moja wapo ya kudumisha matukufu ya heshima
Na watoto wanapo fikia umri wa kubaleghe basi nawatake ruhusa, kama walivyo taka ruhusa wa kabla yao. Hivyo ndivyo anavyo kubainishieni Allah Aya zake, na Allah ni Mjuzi Mwenye hekima
ANNUUR
59
Kuomba idhini ya kuingia katika nyumba si tabia tu ya kijamii, bali ni malezi ya kiimani yanayo takiwa kuwafundisha watoto namna ya kuheshimu watu wengine tangu utotoni mwao.