Uhuru si kusema utakalo, bali ni kusema haki bila ya woga wala matamanio
Kumtii Allah si unyonge, bali ndiyo njia pekee ya kupata mafanikio makubwa
Uhuru katika Qur'ani
Kujisalimisha maisha yako kwa ajili ya Allah kwa kutii ndiyo uhalisia wa uhuru, kwa sababu wewe mwenyewe utakuwa umechagua njia ya amani.
Mwenye uhuru halisi ni yule mwenye kuutakasa moyo wake kwa ajili ya Allah, na siyo kwa ajili ya watu
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehemu
Enyi mlio amini! Mcheni Allah na
semeni maneno ya sawa sawa
Apate kukutengenezeeni vitendo
vyenu na akusameheni madhambi
yenu. Na anaye mt'ii Allah na
Mtume wake, bila ya shaka
amefanikiwa mafanikio makubwa
[AL-AHZAAB 70:71 ]
Uhuru si kusema utakalo, bali ni kusema haki bila ya woga wala matamanio.
Maneno mazuri ndiyo sauti itokayo katika moyo wa mtu anaye muogopa Allah kabla ya kutamka.
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehemu
Enyi mlio amini! Mcheni Allah na
semeni maneno ya sawa sawa
Apate kukutengenezeeni vitendo
vyenu na akusameheni madhambi
yenu. Na anaye mt'ii Allah na
Mtume wake, bila ya shaka
amefanikiwa mafanikio makubwa
[AL-AHZAAB 70:71 ]
Mwenye kumnyenyekea Allah huwa huru kutokana na udhalili wa kuwahofu viumbe.
Kumtii Allah si unyonge, bali ndiyo njia pekee ya kupata mafanikio makubwa.
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehem
Basi kimbilieni kwa Allah hakika mimi
kwenu ni muonyaji wa wazi
Na msifanye kinyume cha Allah mungu
mwingine mimi kwenu ni muonyaji
mbainishaji kutoka kwake
[ ADH-DHAARIYAAT 50:51 ]
Uhuru wa kweli ni kujitenga na utumwa wa dunia kwa kuelekea kwenye rehema za Allah.
Amesema Allah Mtukufu: “Basi kimbilieni kwa Allah”.
Basi, hakuna sehemu ya kuukimbilia uhuru isipokuwa kwake tu.
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehem
Basi kimbilieni kwa Allah hakika mimi
kwenu ni muonyaji wa wazi
Na msifanye kinyume cha Allah mungu
mwingine mimi kwenu ni muonyaji
mbainishaji kutoka kwake
[ ADH-DHAARIYAAT 50:51 ]
Upendo wowote usio kuwa kwa ajili ya Allah una ukomo maalumu.
Na kumpwekesha Allah pekee, ndiyo kwenye mafanikio ya milele.
Basi, usimfanye mungu mwingine pamoja na Allah, utakuwa ndiye mja mwenye uhuru wa kweli.
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehemu
Na mwenye kuuelekeza uso wake kwa Allah,
naye akawa anafanya wema, basi huyo
hakika amekwisha kamata fundo lilio
madhubuti. Na mwisho wa mambo yote ni
kwa Allah
Na anaye kufuru, isikuhuzunishe kufuru
yake. Kwetu ndio marudio yao, na hapo
tutawaambia waliyo-yatenda. Hakika Allah
ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani
[LUQMAAN 22:23]
Kujisalimisha maisha yako kwa ajili ya Allah kwa kutii ndiyo uhalisia wa uhuru, kwa sababu wewe mwenyewe utakuwa umechagua njia ya amani.
Mwenye uhuru halisi ni yule mwenye kuutakasa moyo wake kwa ajili ya Allah, na siyo kwa ajili ya watu.
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehemu
Na mwenye kuuelekeza uso wake kwa Allah,
naye akawa anafanya wema, basi huyo
hakika amekwisha kamata fundo lilio
madhubuti. Na mwisho wa mambo yote ni
kwa Allah
Na anaye kufuru, isikuhuzunishe kufuru
yake. Kwetu ndio marudio yao, na hapo
tutawaambia waliyo-yatenda. Hakika Allah
ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani
[LUQMAAN 22:23]
Mwenye kuyaweka maisha yake kwa Allah, hato babaika na changamoto yoyote ya maisha , wala ukafiri wowote wa makafiri.
Uhuru wa kweli ni wewe kujua kuwa marejeo yako yapo kwa Allah tu pekee.
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehemu
Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako
Mlezi. Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae.
Hakika Sisi tumewaandalia wenye kudhulumu
Moto ambao utawazunguka kama khema. Na
wakiomba msaada watasaidiwa kwa kupewa maji
kama mafuta yaliyo tibuka. Yatakayo wababua
nyuso zao. Kinywaji hicho ni kiovu mno! Na
matandiko hayo ya kupumzikia ni maovu mno
[AL-KAHF 29]
Uislamu haumlazimishi mtu kuamini, bali unatangaza haki kwa uwazi kwa kusema:
“Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae”.
Uhuru katika uislamu ni uhuru wa kutafuta ukweli, siyo kuukimbia.
MAZINGATIO:
Uhuru ni maamuzi ya kuchagua, kwani haki inatoka kwa Mola wenu Mlezi tu.
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehemu
Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako
Mlezi. Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae.
Hakika Sisi tumewaandalia wenye kudhulumu
Moto ambao utawazunguka kama khema. Na
wakiomba msaada watasaidiwa kwa kupewa maji
kama mafuta yaliyo tibuka. Yatakayo wababua
nyuso zao. Kinywaji hicho ni kiovu mno! Na
matandiko hayo ya kupumzikia ni maovu mno
[AL-KAHF 29]
Imani hainunuliwi wala hailazimishwi, bali huchaguliwa na moyo, wakati moyo huo unapojua uzuri wa haki.
Lakini uhuru bila ya kutekeleza majukumu yake hubadilika na kuwa majuto baada ya muda kupita.
MAZINGATIO:
Uhuru wa kweli ni kuchunga majukumu katika utashi.
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehemu
Hakuna kulazimisha (watu
kuingia) katika dini. Hakika,
uongofu umekwishajitenga na
upotovu. Basi anayemkataa
Twaghuti na kumuamini Allah,
bila shaka yeye ameshika
kishikio madhubuti
kisichovunjika. Na Allah ni
Mwenye kusikia sana, Mjuzi sana
[AL-BAQARAH 256]
“Hakuna kulazimisha katika Dini” siyo alama tu ya dini ya Uislamu, bali ndiyo ukweli wa Qur’an.
Uislamu unakuita ili utafakari mwenyewe, bila kukulazimisha.
Kwani, haki ipo wazi kwa kila mwenye kutaka kuiona.
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehemu
Hakuna kulazimisha (watu
kuingia) katika dini. Hakika,
uongofu umekwishajitenga na
upotovu. Basi anayemkataa
Twaghuti na kumuamini Allah,
bila shaka yeye ameshika
kishikio madhubuti
kisichovunjika. Na Allah ni
Mwenye kusikia sana, Mjuzi sana
[AL-BAQARAH 256]
Uhuru wa kweli ni wewe kuwa huru na utumwa wa kuwadhalilikia viumbe na fikra potofu, na kisha ukamuamini Allah peke yake.
Unapomkufuru shetani na kumuamini Muumbaji, unakuwa umeshikamana na kamba madhubuti isiyo katika.
Sema: Enyi watu, hakika imekujieni haki
kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi
yeyote anayeongoka, anaongoka kwa
faida ya nafsi yake, na anayepotea, basi
kwa hakika anapotea kwa hasara ya
nafsi yake. Na mimi si msaidizi kwenu
[YUNUS 108 ]
Mpe kila mtu haki kwa ajili ya Allah, kisha acha utashi wa maamuzi kwa kila nafsi.
Mwenye kufuata uongofu,basi ni kwa faida yake mwenyewe, na mwenye kuupuuza hujidhuru mwenyewe.
Sema: Enyi watu, hakika imekujieni haki
kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi
yeyote anayeongoka, anaongoka kwa
faida ya nafsi yake, na anayepotea, basi
kwa hakika anapotea kwa hasara ya
nafsi yake. Na mimi si msaidizi kwenu
[YUNUS 108 ]
Mtume hakutumwa kuja kuwalazimisha watu kuamini, bali kuufikisha ujumbe wa Allah.
Na kila mtu ana uhuru wa kuchagua njia yake yeye mwenyewe itakayo mfikisha mbele ya Allah.
Huu ndiyo uhuru ambao hauiondoshi imani, bali unaikamilisha.
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehemu
Waite (walinganie watu) katika njia
ya Mola wako kwa hekima na
mawaidha mazuri, na ujadiliane nao
kwa namna iliyo bora. Hakika Mola
wako mlezi yeye anamjua zaidi
aliyepotea katika njia yake, na yeye
ndiye anayewajua zaidi walioongoka
[ANNAHLI 125 ]
Qur’an haiwaiti watu kugombana, bali inawaita watu kujadiliana kwa kutumia hekima.
“Na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora”.
Hili ni daraja liliojengwa kutokana na maneno mazuri yenye kutengeneza mambo yaliyo haribiwa kutokana na ugumu wa nyoyo.
MAZINGATIO:
Majadiliano yenye kuleta ufanisi huongozwa na hekima
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehemu
Waite (walinganie watu) katika njia
ya Mola wako kwa hekima na
mawaidha mazuri, na ujadiliane nao
kwa namna iliyo bora. Hakika Mola
wako mlezi yeye anamjua zaidi
aliyepotea katika njia yake, na yeye
ndiye anayewajua zaidi walioongoka
[ANNAHLI 125 ]
Majadiliano katika uislamu siyo vita, bali ni wito wa kuziweka pamoja akili na nyoyo ili kuungana katika mwanga wa haki.
Mwenye kuamini na kushikamana na hekima, basi ataamini na kutambua kuwa maneno mazuri ndiyo yenye nguvu kuliko silaha.
MAZINGATIO:
Kujenga daraja la majadiliano ndiyo adabu nzuri ya kuondoa ikhitalafu
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehem
Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu
kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye
baina yako na baina yake pana uadui
atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea
uchungu
Lakini hawapewi wema huu ila wanao
subiri, wala hawapewi ila wenye bahati
kubwa
[FUSSWILAT 34:35]
Unapo kabiliana na ubaya kwa kufanya wema, huwa unavunja kuta za chuki na kujenga daraja la mahusiano bora.
Qur’an inatufundisha kuwa, nyoyo hufunguliwa kwa upole siyo kwa nguvu.
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehem
Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu
kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye
baina yako na baina yake pana uadui
atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea
uchungu
Lakini hawapewi wema huu ila wanao
subiri, wala hawapewi ila wenye bahati
kubwa
[FUSSWILAT 34:35]
Majibu mazuri hayatoki isipokuwa kwenye nafsi yenye heshima kubwa na subira kubwa.
Mtu anapo shikamana na adabu hizo, humfanya avuke vizingiti vya uadui na kufikia kwenye kilele cha utu wa hali ya juu.
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehem
Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake
zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu
kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina
yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara
kwa watu wanao fikiri
[ARRUUM 21]
Katika mfumo wa Qur’an ndoa si mafungamano ya kawaida, bali ni mafungamano ya utulivu, upendo na huruma.
Aya haimzungumzii mume na mke tu, bali inazungumzia kuhusu nyoyo mbili zilizo ungana kwa ajili ya Allah na kuleta mshikamano wa kweli katika jamii.
MAZINGATIO:
Qur’an na malezi ya familia ni kujengwa juu ya upendo na huruma.
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehem
Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake
zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu
kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina
yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara
kwa watu wanao fikiri
[ARRUUM 21]
Allah anapojaalia ndani ya nyoyo kukawa kuna upendo na huruma, basi nyumba huwa ni pepo ndogo duniani.
Upendo katika Uislamu si tabia tu ya kuzuka, bali ni alama kubwa miongoni mwa alama za Muumbaji.
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehem
Na Mola wako Mlezi ameam-risha kuwa msimuabudu
yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwa-tendee wema.
Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote
wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na
sema nao kwa msemo wa heshima
Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea
huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama
walivyo nilea utotoni
[AL-ISRAA 23:24 ]
Qur’an kabla haijaamrisha sala, imeusia kuwafanyia wema wazazi.
Kwani kuwafanyia wema wazazi siyo tu ni uzuri tunao urudisha, bali ni shukurani ya maisha inayo tuzawadia baraka ya kila kitu.
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehem
Na Mola wako Mlezi ameam-risha kuwa msimuabudu
yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwa-tendee wema.
Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote
wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na
sema nao kwa msemo wa heshima
Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea
huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama
walivyo nilea utotoni
[AL-ISRAA 23:24 ]
Wema hauhitaji kufanya mambo makubwa, wakati mwingine wema huwa ni kusema neno zuri tu inatosha.
Qur’an tukufu imetufundisha kuwa kuonesha “mguno” tu husababisha kuleta maudhi ndani ya nyoyo za wazazi.
Na kuwahurumia ni dalili kubwa ya kuonesha shukurani kwao.
MAZINGATIO:
Kuwafanyia wema wazazi ni mwenendo bora wa Qur’an.