Na msiwaoe wale walio olewa na baba zenu ispokuwa yaliyopita, tendo hilo ni baya na bughdha na ni njia mbaya
Wameharamishwa kwenu mama zenu, na binti zenu na dada zenu na shangazi zenu, na ndugu wa mama zenu na watoto wa kaka zenu, na watoto wa dada zenu, na mama zenu ambao wamewanyonyesha na dada zenu wa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wa wake zenu ambao wapo majumbani mwenu wanaotokana na wake mlio waingilia, kama (wake hao) hamjawaingilia, basi sivibaya kwenu . Na (ni haramu kwenu) wake wa watoto wenu wa kuwazaa na (ni haramu) kuwakusanya mtu na dada yake ispokua yale yaliyopita, hakika Allah ni mwenye kusamehe mpole mno
Kadi zenye uhusiano
Tazama kadi