Mashindano yoyote yana upeo na ukomo wake.
Na uhai pia upo hivyo hivyo, hakuna kisicho kuwa na mwisho.
Tazama kadi
Watu wengi wanamuheshimu mchezaji anayepambana bila kujisalimisha kirahisi rahisi. Na Qur’an pia inamfundisha mwanaadam namna ya kusubiri katika changamoto mbalimbali na kuendelea na njia ya mafanikio bila kukata tamaa!
“Na maisha ya dunia si kitu il ani starehe ya udanganyifu
Mamilioni ya watu hushuhudia mashindano mbali mbali kutokea maeneo tofauti tofauti ya dunia. Lakini mwanaadam anabakia kuwa na haja ya kupata anayemsikia na kumfahamu kweli katika mihangaiko yake.
“Hakika kwa kumkumbuka Allah ndio nyoyo hutua!”.
Mchezaji wakati mwingine anashindwa kwenye mashindano, kisha anarudi tena kwa nguvu kubwa. Hivyo hivyo, hata mwanadam anaweza kuanza upya katika harakati zake za maisha anapokutana na changamoto yoyote. Tambua kuwa Qur’an haijaufunga mlango wa matumaini, hivyo usikate tamaa!
Baadhi ya ushindi hauji kwa haraka. Na katika maisha hli ni hivyo hivyo, subira ni sehemu ya safari ya mafanikio.