“Na maisha ya dunia si kitu il ani starehe ya udanganyifu
Tazama kadi
Nyuma ya nguvu tunazoziona kwenye michezo mbali mbali, kuna mwanadam anaye choka na kuwa na hofu na kudhoofika. Na Qur’an inamzungumzia mwanadam katika hali ukweli na huruma kuhusu maumbile yake.
Kila mashindano duniani yana lengo maalumu. Je,inawezekanaje kiakili iwe maisha ya mwanaadam pekee hapa duniani yawe bila maana (lengo)?
Watu wengi wanamuheshimu mchezaji anayepambana bila kujisalimisha kirahisi rahisi. Na Qur’an pia inamfundisha mwanaadam namna ya kusubiri katika changamoto mbalimbali na kuendelea na njia ya mafanikio bila kukata tamaa!
Katika kila mashindano huwa kuna hofu inayo jitokeza kabla ya mwisho. Na katika maisha, hali hiyo pia ipo. Moyo huwa na kawaida ya kutafuta kitu kitakacho upa amani ya kweli daima
“Hakika kwa kumkumbuka Allah ndio nyoyo hutua!”.
Katika kombe la dunia, kuna tofauti ya rangi, lugha na nchi, lakini wote hao wanabaki katika ubinaadam wao. Basi, tambua kuwa Qur’an inatukumbusha kulinda heshima ya kila mtu.