Je! Hawaizingatii hii Qur’ani? Au kwenye nyoyo (zao) zipo kufuli?
Tazama kadi
Ambao uwapatapo msiba husema: Hakika, sisi ni wa Allah, na kwake yeye tu tutarejea
Qur’an si gumzo la lugha au kundi fulani, bali ni muongozo na ponyo ya kila moyo wenye imani. Na mwenye kuipuuza atabaki masafa marefu kati yake na haki, masafa ambayo hayafikiki. MAZINGATIO: Qur’an ni muongozo wa walimwengu.
Qur’an imekuwa ni neema ya kwanza baada ya rehema za Allah. Na inatufunza kuwa neema kubwa aliyo fundishwa mwanaadam baada ya kuumbwa kwake ni kupewa ujuzi wa maneno ya Allah (Qur’an). MAZINGATIO: Qur’an ni rehema.
Nyoyo ndiyo zinazo fahamu, siyo masikio. Basi, yeyote mwenye kuufungua moyo wake kwa kuifuata haki, atapata katika Qur’an nuru. Na mwenye kuufunga moyo wake, basi hautosikia chochote, hata kama atasomewa Aya zote. MAZINGATIO: Nyoyo ndiyo husikia na kuzingatia.
Enyi mlioamini, ombeni msaada kwa uvumilivu (subra) na kuswali. Bila shaka, Allah yupo pamoja na wenye uvumilivu
Na kwa yakini kabisa, tutakutieni katika mtihani mdogo wa hofu na njaa na upungufu wa mali na uhai na matunda. Na wape bishara wenye uvumilivu