Na simamisheni mzani kwa uadilifu na msipunguze mizani
Tazama kadi
Na kwa yakini Tumemuumba Mtu na Tunajua yale inayowaza nafsi yake, na Sisi Tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake
Hakika amefanikiwa aliye itakasa, Na hakika amepata hasara aliye iviza (ichafua)
Allah, hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye tu. Yeye ndiye Mwenye uhai wa milele, Mwenye kusimamia kila kitu. Hapatwi na kusinzia wala kulala. Ni vyake yeye tu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Ni nani awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, wala hawajui kitu katika elimu yake is...
Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti aliye wakilishwa juu yenu; kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu Mlezi
Kwa hakika Allah anaamuru uadilifu, na ihsani, na kuwapa (sadaka) ndugu wa karibu na anakataza uchafu, na uovu, na uasi. Anawanasihini ili mpate kukumbuka
Hakika, Allah anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe, na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika, mazuri mno anayokuwaidhini Allah ni hayo. HakikaAllah ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona