Alikuwa Zakariya kila anapoingia kwa Mariam hukuta riziki ya matunda, alipomuuliza kuhusu matunda hayo alijibu kwa uwazi: (Riziki hii yatoka wa Allah). Hivi ndivyo kinavyoanza kisa cha Mariam katika Qur’ani … kwa moyo unaofahamu kuwa riziki ya Allah inaweza kuja pasina binadamu kutarajia.
Kabla ya Issa kuzaliwa, Mariam alijiwa na habari: (Jina lake ni Masihi Issa mwana wa Mariam). Na Qur’ani inamsifu kwamba yeye ni mwenye hishima katika dunia na akhera na miongoni mwa waliowekwa karibu na Allah. Kwa ajili hiyo huwezi kufahamu mtazamo wa uislamu juu ya Issa pasina kusoma kisa cha Mariam.