Uislamu haukutaki kutokuwa na udhaifu, bali unakutaka kujua ni nani wa kumtegemea unapo dhoofika
Tazama kadi
Ulimwengu unawafauatilia wachezaji katika kombe la dunia. Lakini Qur’an inakutaka ujiangalie wewe mwenyewe kwanza.
Nyuma ya nguvu tunazoziona kwenye michezo mbali mbali, kuna mwanadam anaye choka na kuwa na hofu na kudhoofika. Na Qur’an inamzungumzia mwanadam katika hali ukweli na huruma kuhusu maumbile yake.
Katika kipindi cha upweke au hofu, Qur’an inazungumza jinsi Allah alivyo karibu na mwanaadam, hivyo asikate tamaa na rehema zake!
Qur’an inamkumbusha mwanaadam kitu ambacho hukisahu sana anapojishughulisha: kwamba safari ni fupi, na maana halisi ya uhai ni muhimu kuizingatia kuliko kujishughulisha na mihangaiko yenye kumalizika ghafla
Kila mashindano duniani yana lengo maalumu. Je,inawezekanaje kiakili iwe maisha ya mwanaadam pekee hapa duniani yawe bila maana (lengo)?
“Hakika kwa kumkumbuka Allah ndio nyoyo hutua!”.