Na kwa yakini kabisa, tumemuumba mtu kutokana na asili ya udongo (halisi)(13)Kisha tukamjaalia awe tone la mbegu ya uzazi iliyokaa katika (sehemu) madhubuti(14)Kisha tukaliumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Allah Mbora wa waumbaji
Kadi zenye uhusiano
Tazama kadi
