Je! Umemwona aliye yafanya matamanio yake kuwa ndio mungu wake? Basi je, wewe utakuwa ni wakili wake?
Tazama kadi
Na wanapo sikia upuuzi hujitenga nao na husema: Sisi tuna vitendo vyetu, na nyinyi mna vitendo vyenu. Salamun Alaikum, Amani juu yenu! Sisi hatutaki kujibizana na wajinga
Pepo si ya mwenye kuzuia hasira zake tu, bali ni ya mwenye kutoa katika wasaa na dhiki, na akawasamehe watu. Njia za kupata radhi za Allah zipo katika matendo ya wema.Tunajifunza kuwa: Huruma ni katika matendo ya wema.
Tunapopatwa na changamoto, na kumtegemea Allah kwa kumuomba Yeye kwa utakaso (Ikhlaswi), basi faraja yake huja haraka bila ya kutegemea. Lakini jambo jema ni kutekeleza shukurani kwa kumuabudu Allah baada ya wokovu na kutozama katika uovu na ujeuri. Tunajifunza kuwa: Kutimiza wajibu ni kumshukuru Allah.
Na ukimbilieni msamaha wa Mola wenu Mlezi na Pepo (ambayo) upana wake ni mbingu na ardhi, iliyoandaliwa kwa ajili ya wacha Mungu (Wacha Mungu) Ambao wanatoa (katika vile walivyopewa na Allah) katika hali ya wasaa na katika hali ya dhiki, na wenye kuzuia hasira (zao) na kusamehe watu (wanaowakosea). Na Allah anawapenda wafanyao mazuri
Kuukimbilia msamaha wa Allah na Pepo yake aliyo waahidi Waumini, ni neema kubwa ya Allah ambayo humpa amtakaye. Basi, ewe Muumini! Weka lengo lako kuu kuwa ni kufaulu kwa kufanya juhudi zitakazo kuwezesha kupata radhi za Allah na kupata msamaha wake. Tunajifunza kuwa:
Kimbilieni kuomba msamaha kwa Mola wenu na Pepo (ambayo) upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, imeandaliwa kwa wale walio muamini Allah na Mtume Wake. Hiyo ni fadhila ya Allah, Humpa Amtakaye. Na Allah ni Mwenye fadhila kubwa