Hakika walio amini na wakatenda mema Arrahmani Mwingi wa Rehema atawajaalia mapenzi
Tazama kadi
Na siku tutakayomfufua shahidi (Mtume) katika kila umma kutoka miongoni mwao atakayethibitisha (kuwa aliwafikishia ujumbe wa Allah wakampinga), na tutakuleta wewe kuwa shahidi wa (watu) hawa. Na tumekuteremshia kitabu kikibainisha kila kitu, na rehema na bishara kwa Waislamu
Heshima kubwa ya Mwanaadam ni yeye kuwa mwenye kupendeza mbele ya Allah, kabla ya kupendwa na yeye. MAZINGATIO: Allah huwapenda waumini, nao wanampenda
Hakuna dhiki yoyote inayopatikana katika moyo isipokuwa Qur’an inayo ubainifu wake, au muongozo, au rehema. MAZINGATIO: Qur’an ni muongozo na rehema
Kumpenda Allah si kwa kudai tu, bali huwa kwa utashi wa moyoni unaobadilisha vipaumbele, na kuupa moyo uhuru wa kutofungamana na mambo yasiyo faa. MAZINGATIO: Ni wajibu kuufunganisha moyo na imani.
Moyo unapo jaa mapenzi ya kumpenda Allah, basi vitu vyote huwa vidogo katika mapenzi yake, na mizani ya mapenzi ya kweli husimama ipasavyo. MAZINGATIO: Kumpenda Allah ndiyo mapenzi ya kweli.
Na miongoni mwa watu kuna wanaofanya washirika badala ya (kumuamini) Allah (pekee); wanawapenda kama wampendavyo Allah. Na walioamini wanampenda zaidi Allah. Na laiti waliodhulumu wangejua watakapoiona adhabu kwamba, nguvu zote ni za Allah, na kwamba, Allah ni mkali wa kuadhibu