Enyi mlio amini! Rukuuni na msujudu, na muabuduni Mola wenu Mlezi, na tendeni mema, ili mfanikiwe
Tazama kadi
Kila kisa katika Qur’an kimebeba masomo kwetu ya kweli katika maisha. Kwa kila mwenye kumuamini Allah atapata kwenye kila Aya muongozo na rehma. MAZINGATIO: Qur’an ni muongozo na masomo ya kimaisha.
Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa (kiongozi) katika ardhi. Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio yakakupoteza kwenye Njia ya Allah. Hakika wanao ipotea Njia ya Allah wakaiacha, watapata adhabu kali kwasababu ya kusahau kwao Siku ya Hesabu
Kila nafsi itavuna ilicho chuma. Na mateso ya duniani ni matokeo ya dhulma za mwanaadam kujidhulumu mwenyewe. Allah hamdhulumu yeyote, lakini watu ndiyo wanaojidhulumu wenyewe. MAZINGATIO: Uadilifu wa Allah na hatari ya dhulma.
Usidai kuwa unatengeneza hali ya kuwa unapandikiza uharibifu (ufisadi). Mwanadamu anatakiwa kufikiria na kupima matendo yake kabla ya kujiridhisha kuwa anayo yafanya ni kheri. MAZINGATIO: Kuwa na fikra nzuri katika kutenda mema
Katika visa vya Mitumekuna mazingatio makubwa kwetu sisi wote. Ndani yake kuna ukumbusho wa kuzingatia na mafundisho kwa yaliyo tokea kwa wale walio tangulia. Qur’an siyo kitabu cha mazungumzo tu, bali ni kitabu cha ukweli, muongozo na rehma. MAZINGATIO: Ni muhimu kuwa na mazingatio katika visa vya wale walio tutangulia
Utafika muda wa kila mtu kuona uhalisia wa mambo kwa uwazi, lakini hapatokuwa na muda wa kutenda mema tena! Yakini ya kweli ni kuamini mwenyewe kwa hiyari kabla ya kufika muda wa kulazimika kuamini hali ya kuwa imani hiyo haitosaidia chochote. MAZINGATIO: Ni muhimu kuwa na yakini ya siku ya kiama.