Hakika walio amini na wakatenda mema Arrahmani Mwingi wa Rehema atawajaalia mapenzi
Tazama kadi
Muda mfupi tu wa kushikamana na haki, ulibadilisha historia ya wachawi, wakawa ni miongoni mwa waumini wenye kusujudu na kumuabudu Allah. MAZINGATIO: Ni muhimu kuzingatia visa vyenye uongofu
Moyo unapo jaa mapenzi ya kumpenda Allah, basi vitu vyote huwa vidogo katika mapenzi yake, na mizani ya mapenzi ya kweli husimama ipasavyo. MAZINGATIO: Kumpenda Allah ndiyo mapenzi ya kweli.
Wakati kifua chako kinapopata dhiki na ukawa hujui ni ipi sababu ya machungu ya dhiki hiyo,yaliyomo ndani yake, basi Qur’an inakuja kukupa suluhisho lake na si kukukaripia. Bali inakuponya maradhi yote uliyo nayo yasiyo onekana kwa macho wala fikra za kawaida. MAZINGATIO: Qur’an ni ponyo la nyoyo
Ujumbe wa Qur’an haubadilishi tu anuani, bali unamuokoa mwanaadam kutokana na ujinga. MAZINGATIO: Ujumbe wa Qur’an ni suluhisho la matatizo yote.
Katika ulimwengu uliofunikwa na giza, Qur’an inakuja kama nuru isiyo kutelekeza, bali inkujulisha njia yenye usalama na amani. MAZINGATIO: Qur’an ndiyo njia ya amani
Mussa tena akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimeza walivyo vizuaHapo wachawi walipinduka wakasujuduWakasema: Tunamuamini Mola Mlezi wa walimwengu wote