Basi Allah Atawakinga na shari ya siku hiyo,"

Basi Allah Atawakinga na shari ya siku hiyo,"

Basi Allah Atawakinga na shari ya siku hiyo,"

17 14

Basi Allah Atawakinga na shari ya siku hiyo, na Atawapa nuru na kuwakutanisha na uchangamfu na furaha(12)Na Atawalipa kwasababu ya kusubiri kwao, Pepo na nguo za hariri(13)Humo wataegemea juu ya viti vya enzi, hawataona (hawatahisi) humo jua kali wala baridi kali.[1](14)Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yataning’inia mpaka chini(15)Na watazungushiwa vyombo vya fedha, na bilauri zilokuwa za vigae
(16)Vigae safi kutokana na fedha wamezipima kwa kipimo(17)Na humo watanyweshwa kinywaji kilicho changanyika na tangawizi
(18)Hiyo ni chemchem iliyo humo inaitwa Salsabil(19)Na watawazungukia wavulana wasio pevuka wakiwatumikia, ukiwaona utadhani ni lulu zilizo tawanywa(20)Na utakapo yaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa(21)Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya atilasi. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao atawanywesha kinywaji safi kabisa(22)(Wataambiwa) Hakika haya ni malipo yenu; na juhudi zenu zimekubaliwa

Kadi zenye uhusiano

Tazama kadi

icon

Shiriki