Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti aliye wakilishwa juu yenu; kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu Mlezi
Tazama kadi
Hakika, Allah Hadhulumu uzito wa punje. Na kama (uzito huo wa punje) ni jambo zuri analizidisha na anatoa ujira mkubwa kabisa kutoka kwake
Na kwa yakini Tumemuumba Mtu na Tunajua yale inayowaza nafsi yake, na Sisi Tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake
Na simamisheni mzani kwa uadilifu na msipunguze mizani
Hakika, sisi tumemuongoza (tumempa mwongozo unaofikishwa na Mitume); ama awe mwenye kushukuru au mwenye kukufuru
Kwa hakika Allah anaamuru uadilifu, na ihsani, na kuwapa (sadaka) ndugu wa karibu na anakataza uchafu, na uovu, na uasi. Anawanasihini ili mpate kukumbuka
Enyi miloamini, kuweni wasimamizi (wa haki) kwa ajili ya Allah, mtoao ushahidi kwa uadilifu. Na kuwachukia (watu) kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu (kwa watu wote). Hilo ndilo lililo karibu zaidi (kufikisha) kwenye uchamungu. Na mcheni Allah. Hakika, Allah anayajua mnayoyatenda