Na wale (wenye akili ndio) ambao huyaunga aliyoamrisha Allah yaungwe, na wanaihofu hesabu mbaya
Tazama kadi
Watakapokujia wanafiki wanasema: Tunashuhudia kwamba wewe bila ya shaka yoyote ni Mtume wa Allah. Na Allah Anajua kuwa hakika wewe ni Mtume Wake, na Allah anashuhudia kuwa kwa hakika kabisa wanafiki ni waongo
Kumfanyia wema jirani ni miongoni mwa tabia njema zilizo sisitizwa na dini yetu tukufu ya Uislamu.Haki za jirani, haziishii kwa jirani aliye ndugu tu, bali zimekusanya hata jirani wa mbali. Hivyo basi, ni wajibu wetu kuzifanya rehema za Allah na uadilifu wake ndiyo msingi wa kuamiliana kwetu katika maisha yetu ya kila siku.Tunachojifunza...
Allah Mtukufu ametuumba mataifa na makabila mbali mbali ili tujuane sisi kwa sisi. Kutofautiana kimaumbile na kimaeneo ni neema, na si sababu ya kutengana. Bali iwe ni msingi wa kuboresha mahusiano yetu kwa kuheshimiana na kutambuana. Tunachojifunza: Kuishi pamoja kwa amani, na kuthaminiana kibinaadamu ni katika Uislamu.
Ukweli ni njia ya wokovu Tunatakiwa kushikamana na wakweli, kwani ndiyo salama ya nyoyo zetu na ukweli wa maneno: “ Mcheni Allah, na kuweni pamoja na wakweli” ili muishi maisha yaliyo jaa baraka na uongofu. Tunachojifunza: Umuhimu wa Ukweli, toba na imani
Na wajizuilie na machafu wale wasiopata cha kuolea, mpaka Allah awatajirishe kwa fadhila yake. Na wanao taka kuandikiwa uhuru katika wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki, basi waandikieni kama mkiona wema kwao. Na wapeni katika mali ya Allah aliyo kupeni. Wala msiwashurutishe vijakazi wenu kufanya zina kwa ajili ya kutafuta pato la maisha ya...
Sema: Kwa hakika Mola wangu Mlezi humkunjulia riziki na humdhikisha amtakaye katika waja wake. Na chochote mtakacho kitoa Yeye atakilipa. Naye ni Mbora wa wanao ruzuku