Je! Umemwona aliye yafanya matamanio yake kuwa ndio mungu wake? Basi je, wewe utakuwa ni wakili wake?
Tazama kadi
Kimbilieni kuomba msamaha kwa Mola wenu na Pepo (ambayo) upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, imeandaliwa kwa wale walio muamini Allah na Mtume Wake. Hiyo ni fadhila ya Allah, Humpa Amtakaye. Na Allah ni Mwenye fadhila kubwa
Kuukimbilia msamaha wa Allah na Pepo yake aliyo waahidi Waumini, ni neema kubwa ya Allah ambayo humpa amtakaye. Basi, ewe Muumini! Weka lengo lako kuu kuwa ni kufaulu kwa kufanya juhudi zitakazo kuwezesha kupata radhi za Allah na kupata msamaha wake. Tunajifunza kuwa:
Kujiepusha na upuuzi ni miongoni mwa tabia njema za waja wa Allah. Hivyo, tunawajibika kuwajibu wajinga, wanapo tusemeza ubaya: “Sisi tuna vitendo vyetu na nyinyi mna vitendo vyenu, hatutaki mijadala na wajinga”. Tunajifunza kuwa: Amani ndio njia yetu, na adabu bora ya kujitenga na upuuzi ni amani.
Tunapopatwa na changamoto, na kumtegemea Allah kwa kumuomba Yeye kwa utakaso (Ikhlaswi), basi faraja yake huja haraka bila ya kutegemea. Lakini jambo jema ni kutekeleza shukurani kwa kumuabudu Allah baada ya wokovu na kutozama katika uovu na ujeuri. Tunajifunza kuwa: Kutimiza wajibu ni kumshukuru Allah.
Kukimbilia msamaha wa Allah na Pepo yake tukufu kwa kutoa, kusubiri, kuzuia hasira, ni miongoni mwa sifa za Wachamungu. Na mwenye kusamehe watu hupata mapenzi ya Allah. Tunajifunza kuwa: Kushikamana na tabia hizi njema ni njia ya kupata msamaha wa Allah na Pepo yake.
Matamanio huvutia nyoyo kupenda mali, watoto na vipambo vya dunia(wanawake nk) lakini vyote hivyo ni starehe ya muda tu. Ama marejeo mema yapo kwa Allah kwa kila mwenye kutakasa niya na kufanya juhudi. Tunajifunza kuwa: Kutakasa niya, ndiyo mafanikio ya kweli.