“Hakika kwa kumkumbuka Allah ndio nyoyo hutua!”.
Tazama kadi
Watu hutafuta furaha katika ushindi. Lakini baadhi ya nyoyo hubakia katika hali ya wasiwasi hata baada ya kushinda, kwa sababu utulivu siyo kombe lenye kubebwa, bali ni amani inayo patikana moyoni.
Uislamu haukutaki kutokuwa na udhaifu, bali unakutaka kujua ni nani wa kumtegemea unapo dhoofika
Kila mashindano duniani yana lengo maalumu. Je,inawezekanaje kiakili iwe maisha ya mwanaadam pekee hapa duniani yawe bila maana (lengo)?
Baada ya kuisha mashindano na makelele, mwanaadam hubaki peke yake pamoja na moyo wake tu(kifo), na wakati huo maswali kuhusu ukweli wa maisha yake aliyo yaishi dunini huanza
Katika kila mashindano huwa kuna hofu inayo jitokeza kabla ya mwisho. Na katika maisha, hali hiyo pia ipo. Moyo huwa na kawaida ya kutafuta kitu kitakacho upa amani ya kweli daima
Umaarufu,kupiga kelele za makofi, na mashindano mbali mbali, vyote hivyo huwa ni vivutio vya kuteka nyoyo za watu kwa haraka, lakini havidumu daima.