Nguvu ya kweli haiko katika ukali… bali katika moyo unaojua kuwa mpole.
Watu huvutiwa na huruma na hujiepusha na mioyo migumu.
Scroll
Kitabu Bure
PDF Free Book
Tabia njema na udugu
Usikubali kuacha magomvi yawatenganishe! Undugu kwa ajili ya Allah huleta nguvu kubwa ya mafungamano kwa kueneza uadilifu na usawa.
Basi suluhisheni, mfanye uadilifu, na muwe ni sababu ya kuleta rehema katika maisha ya watu.
Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni wale wanao tembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama! *Na wale wanao kesha kwa ajili ya Mola wao Mlezi kwa kusujudu na kusimama
ALFURQAAN-63-64
Waja wema ni wale wanaotembea kwa staha (utulivu)…
Hawatafuti ushindi katika kila mjadala, wala hawajibu ujinga kwa ujinga.
Nyoyo zao zimechagua amani, kwa sababu kujikurubisha kwa Allah, ni jambo muhimu kwao kuliko kusema sema ovyo!
Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni wale wanao tembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama! *Na wale wanao kesha kwa ajili ya Mola wao Mlezi kwa kusujudu na kusimama
ALFURQAAN-63-64
Kuna watu duniani huwa ni watulivu wakati wa mchana, lakini nyoyo zao huwa hai wakati wa usiku.
Katika kipindi ambacho watu wamelala, basi wao wanasimama usiku mbele ya Allah kwa kumuabudu, kwani katika nyakati hizo ndipo nyoyo njema hutengenezwa.
Basi ni kwa rehema za Allah umekuwa mpole kwao, na lau ungekuwa muovu wa tabia, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangekukimbia, basi samehe na uwaombee msamaha na watake ushauri katika jambo, na ukitia azma ya jambo basi mtegemee Allah, hakika Allah anawapenda wenye kumtegemea
AL-IMRAN-159
Nguvu za kweli hazipatikani katika ususuavu (ugumu) wa moyo.
Bali zipo kwenye moyo unaojua namna ya kulainika.
Siku zote watu huupenda na kuukaribia moyo wenye huruma, na hujitenga na moyo mgumu usio na huruma.
Basi ni kwa rehema za Allah umekuwa mpole kwao, na lau ungekuwa muovu wa tabia, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangekukimbia, basi samehe na uwaombee msamaha na watake ushauri katika jambo, na ukitia azma ya jambo basi mtegemee Allah, hakika Allah anawapenda wenye kumtegemea
AL-IMRAN-159
Kiongozi bora huwa hawatukani watu, bali huwa na tabia ya kusamehe, na kusikiliza na kushauriana katika mambo.
Nyoyo hujengwa kwa tabia hizo njema, kabla ya kujenga maazimio yoyote.
Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allah ni kama mfano wa punje iliyotoa mashuke saba, ikawa katika kila shuke mna punje mia. Na Allah humuongezea amtakaye, Na Allah ni Mwingi wa fadhila, Mjuzi mno
AL-BAQARAH-261
Kutoa sadaka katika mizani ya kidunia huonekana ni kupungukiwa.
Lakini katika mizani ya Allah ni chanzo kikubwa cha wingi wa mafanikio.
Mtu anapotoa punje ndogo tu, basi huenda ikazalisha mashamba mengi ya kheri bila kutegemea.
Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allah ni kama mfano wa punje iliyotoa mashuke saba, ikawa katika kila shuke mna punje mia. Na Allah humuongezea amtakaye, Na Allah ni Mwingi wa fadhila, Mjuzi mno
AL-BAQARAH-261
Uzuri ulioje katika kutoa!
Hakika unapotoa huwezi kuona matunda yake yote, lakini Allah anayaona, na hujaalia kutoka katika vichache na kuwa kheri nyingi zenye kuongezeka maradufu.
MAZINGATIO:
Ukarimu na kujitolea katika kheri ni nuru ya Qur’an.
Wale watoao mali zao usiku na mchana, kwa siri na kwa dhahiri, basi wana malipo yao kwa Mola wao, na hawatakuwa na hofu yoyote na hawatahuzunika
AL-BAQARAH-274
Baadhi ya nyoyo hutoa vipawa vyao kwa siri, hazisubiri kusifiwa wala hazitafuti kuonwa na watu.
Zinatambua kuwa Allah anaziona, na hilo tu linawatosha.
Wale watoao mali zao usiku na mchana, kwa siri na kwa dhahiri, basi wana malipo yao kwa Mola wao, na hawatakuwa na hofu yoyote na hawatahuzunika
AL-BAQARAH-274
Utoaji bora hausubiri muda maalumu, bali huwa wakati wowote, na huwa katika kipindi cha usiku, au mchana, kwa siri au dhahiri.
Moyo unapojawa na mapenzi ya kufanya kheri basi hupata njia ya kuwajali na kuwathamini wengine.
MAZINGATIO:
Ukarimu na kutoa katika mambo ya kheri ni nuru ya Qur’an.
Si jukumu lako kuwaongoa, lakini Allah humuongoa amtakaye. Na heri yoyote muitoayo, basi ni kwa (manufaa ya) nafsi zenu. Na msitoe ila kwa kutafuta wajihi (radhi) za Allah, na heri yoyote mtakayotoa mtarudishiwa kamili, nanyi hamtadhulumiwa
AL-BAQARAH-272
Utoaji bora hausubiri kupata badala, wala hautafuti kustahiki wingi, bali inatosha tu kuwa ni kwa ajili ya Allah.
Basi, fahamu kuwa kila kheri unayoitoa ipo siku manufaa yake yatarudi kwako tu!
MAZINGATIO:
Kuwa na ikhlaswi (utakaso) katika sadaka ni nuru ya Qur’an.
Si jukumu lako kuwaongoa, lakini Allah humuongoa amtakaye. Na heri yoyote muitoayo, basi ni kwa (manufaa ya) nafsi zenu. Na msitoe ila kwa kutafuta wajihi (radhi) za Allah, na heri yoyote mtakayotoa mtarudishiwa kamili, nanyi hamtadhulumiwa
AL-BAQARAH-272
Unapotoa kwa ajili ya Allah fahamu kuwa hupati hasara yoyote.
Kheri yoyote ambayo leo unaitoa kwa mkono wako, ujue kuwa itakurudia mwenyewe ikiwa kamili katika kipindi anachokijua Allah.
Na mwabuduni Allah na msikishirikishe naye kitu chochote. Na wazazi wawili wafanyieni mazuri, na ndugu wa karibu (wa nasaba), na Yatima na maskini na jirani wa karibu (mwenye udugu wa nasaba) na jirani wa mbali (kwa makazi au udugu) na rafiki aliyeko ubavuni (rafiki mwenye usuhuba wa karibu na pia mke) na msafiri (aliyeharibikiwa) na wale walio chini ya mikono yenu ya kuume (watumwa waliopo chini ya miliki yenu). Hakika, Allah hawapendi wenye kiburi, wenye majivuno mengi
ANNISAI-36
Imani haidhihiri katika swala tu, bali inadhihiri katika nyakati tunazo amiliana na watu.
Tunawajibika kuwafanyia wema wazazi, kuwahurumia wanyonge na kuwa wapole kwa kila tunaye kutana naye katika maisha yetu.
MAZINGATIO:
Kujipamba kwa tabia njema na kuwafanyia watu wema ni nuru ya Qur’an.
Na mwabuduni Allah na msikishirikishe naye kitu chochote. Na wazazi wawili wafanyieni mazuri, na ndugu wa karibu (wa nasaba), na Yatima na maskini na jirani wa karibu (mwenye udugu wa nasaba) na jirani wa mbali (kwa makazi au udugu) na rafiki aliyeko ubavuni (rafiki mwenye usuhuba wa karibu na pia mke) na msafiri (aliyeharibikiwa) na wale walio chini ya mikono yenu ya kuume (watumwa waliopo chini ya miliki yenu). Hakika, Allah hawapendi wenye kiburi, wenye majivuno mengi
ANNISAI-36
Kheri kubwa huwa kwa kufanya wema kwa kuanzia na walio karibu yako, nyumbani na kwa ndugu zako na jirani zako.
Moyo unapo jaa wema, basi kheri huenea kila sehemu katika jamii.
Enyi ambao mmeamini wasicheze shere watu miongoni mwa watu huenda wakawa bora kuliko wao, wala wanawake kwa wanawake huenda wakawa bora kuliko wao wala msizidharau nafsi zenu wala msipeane majina mabaya ya uovu baada ya imani, na yeyote asiye tubu basi hao ndio madhalimu
-11 AL-HUJURAAT
Neno la dharau linaweza kuonekana ni dogo, lakini likaleta maumivu makubwa usiyo yaona ndani ya nyoyo.
Hivyo basi, jitahidi sana kuulinda ulimi wako.
Inaweza kuwa unayemdharau akawa ni mchamungu zaidi kuliko wewe mbele ya Allah.
MAZINGATIO:
Kuwa na tabia njema na kuwaheshimu watu ni nuru ya Qur’an.
Enyi ambao mmeamini wasicheze shere watu miongoni mwa watu huenda wakawa bora kuliko wao, wala wanawake kwa wanawake huenda wakawa bora kuliko wao wala msizidharau nafsi zenu wala msipeane majina mabaya ya uovu baada ya imani, na yeyote asiye tubu basi hao ndio madhalimu
-11 AL-HUJURAAT
Nyoyo hujengwa kwa maneno, na huvunjwa kwa maneno pia.
Basi, usiwadharau watu, wala kuwa fedhuli wa maneno, wala usiwaite watu kwa sifa wasio zipenda.
Heshima ni haki ya kila mtu.
MAZINGATIO:
Tabia njema na kusema maneno mazuri ni nuru ya Qur’an
Na endapo makundi mawili yamepigana basi wasuluhisheni kati yao na endapo litaasi moja ya makundi hayo juu ya lingine basi lipigeni ambalo linaasi hadi lirudi kwenye amri ya Allah na endapo litarudi basi wasuluhisheni kati yao kiuadilifu na fanyeni usawa hakika Allah anapenda wenye kutenda usawa
-Hakika waumini ni ndugu basi suluhishaneni kwenye udugu wenu na mumche Allah ili mpate kurehemewa
AL-HUJURAAT -9-10
Waumini ni ndugu!
Na mapenzi hayajengwi kwa magomvi.
Inapotokea sintofahamu baina yenu, basi fanyeni kila linalo wezekana kusuluhisha kwa uadilifu, kwani Allah anawapenda wanaofanya uadilifu baina ya watu.
MAZINGATIO:
Tabia njema na kusuluhisha baina ya watu ni nuru ya Qur’an.
Na endapo makundi mawili yamepigana basi wasuluhisheni kati yao na endapo litaasi moja ya makundi hayo juu ya lingine basi lipigeni ambalo linaasi hadi lirudi kwenye amri ya Allah na endapo litarudi basi wasuluhisheni kati yao kiuadilifu na fanyeni usawa hakika Allah anapenda wenye kutenda usawa
-Hakika waumini ni ndugu basi suluhishaneni kwenye udugu wenu na mumche Allah ili mpate kurehemewa
AL-HUJURAAT -9-10
Usikubali kuacha magomvi yawatenganishe!
Undugu kwa ajili ya Allah huleta nguvu kubwa ya mafungamano kwa kueneza uadilifu na usawa.
Basi suluhisheni, mfanye uadilifu, na muwe ni sababu ya kuleta rehema katika maisha ya watu.
Utengano huleta udhaifu na majanga.
Na umoja wa kweli huziunganisha nyoyo na kueneza huruma kwa watu.
Basi, shikamaneni kwa yale yanayo leta umoja wenu, kwani hii ni neema kubwa isiyopimwa kwa chochote.
Wenzako wanapo hangaika kukutenga, basi usihuzunike, bali Allah pekee anakutosha!
Kwa kushikamana na nguvu ya imani na kumtegemea Allah, nyoyo huungana na upendo wa dhati hushinda udanganyifu.
MAZINGATIO:
Kumtumaini Allah na kushikamana katika umoja ni nuru ya Qur’an.
Mali na juhudi havitengenezi undugu wa kweli.
Bali, Allah pekee ndiye huziwafikisha nyoyo na huziunganisha.
Basi, mtegemee Yeye tu, kwani umoja wa kweli huanzia kwenye moyo wenye imani.