“Je! Wakati haujafika bado kwa walio amini zikanyenyekea nyoy zao kwa kumkumbuka Allah na haki iliyo teremka? Wala wasiwe kama walio pewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu, kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu, na wengi wao wakawa wapotovu”. Surat Al-Hadiid: 16.
Je! ni nyoyo ngapi zilizo jiweka mbali na kumkumbuka Allah, mpaka zikawa ngumu na kususuwaa, hali ya kuwa bado wito wa Allah, Mola Mlezi wa viumbe unawaita na kuzitaka zirudi katika unyenyekevu.
Je! haujafika wakati kwa nyoyo hizo kunyenyekea?
MAZINGATIO:
Umuhimu wa kuzizindua nyoyo kutokana na kujisahau, katika kumkumbuka Allah.
“Je! Wakati haujafika bado kwa walio amini zikanyenyekea nyoy zao kwa kumkumbuka Allah na haki iliyo teremka? Wala wasiwe kama walio pewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu, kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu, na wengi wao wakawa wapotovu”. Surat Al-Hadiid: 16.
Kujisahau kunasababisha nyoyo kuwa ngumu.
Na kumkumbuka Allah kunazilainisha nyoyo na kuzihuisha upya.
Usisubiri kufunikwa na dunia, bali rudi hivi sasa kwa Allah na umuabudu Yeye tu!
“Soma uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Sala. Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumkumbuka Allah ndiyo jambo kubwa kabisa. Na Allah anayajua mnayo yatenda”. Surat Al-Ankaboot: 45.
Qur’an husomwa ili kuzifundisha nyoyo maadili mema.
Na Sala husimamishwa ili kuzisafisha nafsi ziwe na tabia njema.
Basi, mwenye kudumisha mafungamano yake na Mola wake Mlezi, atapata ulinzi wake wa kutokuwa na maadili mabaya.
“Soma uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Sala. Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumkumbuka Allah ndiyo jambo kubwa kabisa. Na Allah anayajua mnayo yatenda”. Surat Al-Ankaboot: 45.
Hakuna katika dunia kitu kikubwa sana kuliko kumkumbuka Allah.
Ni nuru ya nyoyo, na kinga ya nafsi, na ngazi ya kuthibiti katika haki.
Kila unapomkumbuka na kumtaja Allah kwa dhati ya ukweli kabisa, basi utakuwa karibu yake sana!
Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili”. Surat Swaad: 29
Qur’an haikuteremshwa kwa ajili ya mapambo wala kupata baraka tu, bali imeteremshwa ili tuifahamu na kuizingatia, na kufuata muongozo wake katika kila jambo.
Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili”. Surat Swaad: 29
Kila Aya katika Qur’an imebeba ujumbe maalumu. Na kila mwenye kuitumia akili yake na moyo wake katika kuizingatia Qur’an basi atapata nuru na elimu ya ufahamu wa mambo.
“Enyi mlio amini! Takeni msaada kwa kusubiri na Sala. Hakika Allah yu pamoja na wanao subiri”. Surat Al-Baqara: 153.
Allah hamtelekezi mwenye kusubiri, bali huwa pamoja naye katika dhiki zake na masikitiko yake yanayomtoa machozi, na katika kila sijda anayo ifanya mja mwema huwa kuna matarajio makubwa ya msaada wa Allah.
“Wale ambao wakifikwa na msiba husema: Hakika sisi ni wa Allah, na kwake Yeye hakika tutarejea”. Surat Al-Baqara: 153.
Katika vipindi vya misiba, haitakiwi kusema sema maneno ya upuuzi! bali inatosha tu kuzingatia kwa Yakini na kurejea maneno mazuri kwa kusema: “Sisi ni wa Allah, na kwake Yeye tutarejea” ndani ya maneno hayo ndiyo ishara ya kujisalimisha kwa Allah na kuridhia qadar yake na kupata utulivu wa nafsi.
MAZINGATIO:
Umuhimu wa kujisalimisha na kurejea kwa Allah kwa kuridhia qadar yake katika vipindi vya misiba.
“Arrahman, Mwingi wa rehema. Amefundisha Qur’an. Amemuumba mwanaadam. Akamfundisha kubaini”. Surat Ar-Rahman: 1 – 4.
Qur’an imekuwa ni neema ya kwanza baada ya rehema za Allah.
Na inatufunza kuwa neema kubwa aliyo fundishwa mwanaadam baada ya kuumbwa kwake ni kupewa ujuzi wa maneno ya Allah (Qur’an).
“Hakika hii Qur’an inaongoa kwenye yale yaliyo nyooka kabisa, na ina wabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba watapata malipo makubwa”. Surat Al-Israa: 9.
Qur’an ina kuongoa kwenye njia iliyo nyooka.
Si kwa maamrisho tu na makatazo, bali ni muongozo wa maisha yako yote kwa kukupa mafanikio na utukufu.
“Hakika hii Qur’an inaongoa kwenye yale yaliyo nyooka kabisa, na ina wabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba watapata malipo makubwa”. Surat Al-Israa: 9.
Bishara kubwa kwa waumini si kwenye maneno tu, bali pia kwenye ahadi kutoka kwa Allah ya kupata malipo makubwa kwa kila muumini mwenye kufuata njia ya wema.
MAZINGATIO:
Bishara njema ya kufanikiwa kwa Waumini watendao mema.
“Na lau tungeli ifanya Qur’an kwa lugha ya kigeni wangeli sema: kwa nini Aya zake hazikupambanuliwa? Yawaje lugha ya kigeni na Mtume Mwarabu? Sema: Hii Qur’an ni uwongofu na poza kwa wenye kuamini. Na wasio amini umo uziwi katika masikio yao, nayo kwao imezibwa hawaioni. Hao wanaitwa nao wako pahala mbali”. Surat Fusswilat: 44.
Qur’an si gumzo la lugha au kundi fulani, bali ni muongozo na ponyo ya kila moyo wenye imani.
Na mwenye kuipuuza atabaki masafa marefu kati yake na haki, masafa ambayo hayafikiki.
“Na lau tungeli ifanya Qur’an kwa lugha ya kigeni wangeli sema: kwa nini Aya zake hazikupambanuliwa? Yawaje lugha ya kigeni na Mtume Mwarabu? Sema: Hii Qur’an ni uwongofu na poza kwa wenye kuamini. Na wasio amini umo uziwi katika masikio yao, nayo kwao imezibwa hawaioni. Hao wanaitwa nao wako pahala mbali”. Surat Fusswilat: 44.
Nyoyo ndiyo zinazo fahamu, siyo masikio.
Basi, yeyote mwenye kuufungua moyo wake kwa kuifuata haki, atapata katika Qur’an nuru.
Na mwenye kuufunga moyo wake, basi hautosikia chochote, hata kama atasomewa Aya zote.