Huu ni ubainifu kwa watu, na ni uongofu na ni mawaidha kwa wacha Mungu
Tazama kadi
Njia zote zinaweza kukupoteza, isipo kuwa njia moja tu, iliyo dhaminiwa na Allah mwenyewe, alipo sema: “Basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika”. MAZINGATIO: Ni wajibu kufuata mwongozo wa Allah ili kupata mafanikio
Unaweza kuwa hauhitaji mawaidha marefu, bali Aya moja tu, ikaingia kwenye moyo wako ulio kuwa tayari, na ikabadilisha mwenendo wako wa maisha! MAZINGATIO: Moyo wenye Imani huzinduka kwa Qur’an
Kwa hakika kabisa, Waumini (kamili) ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa hofu, na wanaposomewa Aya zake huwaongezea imani, na wanamtegemea Mola wao Mlezi tu
Kuihama Qur’an haimaanishi kuisahau tu, bali kuishi kwa kujiona kuwa Qur’an haituhusu kwa lolote! MAZINGATIO: Usiihame Qur’an!
Qur’an haikuteremshwa ili kuwa mapambio ya vitu, bali imeteremshwa ili kuziongoza nyoyo. Fungua moyo wako kwanza kabla ya kuufungua msahafu wakati wa kuusoma! MAZINGATIO: Ni wajibu kuizingatia Qur’an.
Usiseme: “Qur’an ni ngumu”. Kwani Allah amekwisha kuwepesishia. Si kwa ajili ya kusomwa tu, bali hata kuuongoza moyo wako kwenye mafanikio ya kweli. Anza sasa! Utaona maajabu ya safari ya mafanikio yako. MAZINGATIO: Mafanikio yanapatikana kwa kufuata njia na muongozo wa Qur’an.