Enyi mlio amini! Rukuuni na msujudu, na muabuduni Mola wenu Mlezi, na tendeni mema, ili mfanikiwe
Tazama kadi
Ni nani atakaye tamani kurudi duniani bila ya kujua mafikio yake ya Akhera?! Maisha ya dunia ndiyo fursa nzuri ya kutenda, ambayo haina badala. Matendo yako ya sasa ndiyo yatakuwa kipimo cha mafikio yako katika siku ya ahadi (kiyama). MAZINGATIO: Akhera inahitajia kufikiria kabla ya kujuta.
Katika kipindi ambacho baadhi ya watu wanadai kuwa wanafanya wema, hali ya kuwa kiuhalisia wao ndiyo wanao fanya uharibifu. Haya huyajua ukweli wake kwa uwazi wale wenye kuzingatia mambo. MAZINGATIO: Umuhimu wa kujua ukweli na ufisadi
Na yote haya tunakusimulia miongoni mwa habari za Mitume yale yanayoupa nguvu moyo wako. Na katika haya imekujia haki na mawaidha na ukumbusho kwa waumini
Soma uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Sala. Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumtaja Allah ndilo jambo kubwa kabisa. Na Allah anayajua mnayo yatenda
Usidai kuwa unatengeneza hali ya kuwa unapandikiza uharibifu (ufisadi). Mwanadamu anatakiwa kufikiria na kupima matendo yake kabla ya kujiridhisha kuwa anayo yafanya ni kheri. MAZINGATIO: Kuwa na fikra nzuri katika kutenda mema
Uhalisia wa mambo utakapo bainishwa baada ya muda wake kufika, haitobakia kwa mtu ila ni majuto tu. Kumbuka kuwa imani haitomfaa mtu baada ya muda wa kufanya matendo kuisha, fanya haraka kutenda mema kabla hujasema: “Najuta, laiti ninge……” MAZINGATIO: Kumbuka maisha ya baada ya kifo