Huu ni ubainifu kwa watu, na ni uongofu na ni mawaidha kwa wacha Mungu
Tazama kadi
Kwa hakika kabisa, Waumini (kamili) ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa hofu, na wanaposomewa Aya zake huwaongezea imani, na wanamtegemea Mola wao Mlezi tu
Ee ole wangu! Laiti nisingeli mfanya fulani kuwa rafiki!Amenipoteza, nikaacha Ukumbusho, baada ya kwisha nijia, na kweli Shet’ani ni khaini kwa mwanaadamu Na Mtume alikuwa akisema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wameifanya hii Qur’ani ni yenye kuhamwa
Uovu si kukosa njia, bali ni kwa kuendelea kufuata njia iliyo mbali na mwangaza wa Allah! Basi, fuata uongofu, utapata utulivu daima. MAZINGATIO: Utulivu wa moyo upo katika kufuata uongofu wa Allah.
Siyo lazima ujue kila kitu. Inakutosha tu kuufungua moyo wako. Allah amekiwepesisha Kitabu chake Kitukufu(Qur’an) kwa kila mwenye kutaka mafanikio. MAZINGATIO: Qur’an ni mwangaza kwa mwenye kuutafuta.
Unapo pata kujihisi moyo wako upo katika Aya aidi inapo somwa, basi tambua kuwa wewe upo karibu sana na msaada wa Allah zaidi ya unavyo dhania. MAZINGATIO: Utulize moyo wako katika Qur’an
Qur’an haigongi masikio yako, bali inaugonga moyo wako, ikiwa uta ufungua, basi utasikia mazuri ambayo haujawahi kuyasikia kabla yake! MAZINGATIO: Kuwa mwepesi wa kuisikiliza Qur’an ii unufaike kwayo