Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazi-linde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao. Hakika Allah anazo khabari za wanayo yafanyaNa waambie Waumini wana-wake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasion-yeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au watoto wa kaka zao, au watoto wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafuasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyohusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Allah, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa
Kadi zenye uhusiano
Tazama kadi