“Kisha kwa Mola wenu Mlezi mtarejeshwa
Tazama kadi
Watu hutafuta furaha katika ushindi. Lakini baadhi ya nyoyo hubakia katika hali ya wasiwasi hata baada ya kushinda, kwa sababu utulivu siyo kombe lenye kubebwa, bali ni amani inayo patikana moyoni.
“Na mwanadam ameumbwa dhaifu
Katika kila mashindano huwa kuna hofu inayo jitokeza kabla ya mwisho. Na katika maisha, hali hiyo pia ipo. Moyo huwa na kawaida ya kutafuta kitu kitakacho upa amani ya kweli daima
Hata katika nyakati ngumu, fahamu daima kuwa hupatikana uwanda wa faraja wenye nuru. Na huu ndio ujumbe tunaokumbushwa na Qur’an tukufu
Mwanaadam ni kiumbe wa thamani ambaye haitakiwi kudharauliwa kwa utu wake, au rangi yake au mji wake. Thamani yake ni kubwa kuliko kitu chochote kinachoundwa
Katika kipindi cha upweke au hofu, Qur’an inazungumza jinsi Allah alivyo karibu na mwanaadam, hivyo asikate tamaa na rehema zake!