Matendo bora na maneno bora ni kulingania katika dini ya Allah, na kutenda mema na kuukubali Uislamu.
Ufisadi na Daʿwah: Njia Mbili, Mwisho Mbili
Lau katika uma zilizo pita kusingekuwa na watu wanao kataza uovu katika miji, basi wange angamizwa wote, lakini Allah aliwaokoa wachache miongoni mwao ambao walikuwa wakikataza maovu.
Ewe Allah! Tujaalie katika wenye kufanya vizuri.
“Wanaume wanafiki na wanawake wanafiki, wote ni hali moja.Huamrisha maovu na huyakataza mema, na huifumba mikono yao. Wamemsahau Allah, basi na Yeye pia amewasahau. Hakika wanafiki ndio wapotofu”.
Surat At-Tawba: 67.
Wanaume wanafiki na wanawake wanafiki, wao ndio wanao amrisha maovu, na wanayakataza mema, na huzuia mikono yao kutoa mali, na humsahau Allah, kwa hali hiyo Allah naye huwalipa kwa kutowajali na kuwatelekeza wakizama katika upotofu wao na kuwaingiza katika adhabu kali siku ya kiama.
MAZINGATIO:
Tahadhari ya unafiki na wanafiki, na kuhakikisha tunashikamana na Uislamu.
“Wanaume wanafiki na wanawake wanafiki, wote ni hali moja.Huamrisha maovu na huyakataza mema, na huifumba mikono yao. Wamemsahau Allah, basi na Yeye pia amewasahau. Hakika wanafiki ndio wapotofu”.
Surat At-Tawba: 67.
Mwenye kuzuia mkono wake kwa kutofanya kheri na akafanya maovu, basi huyo ndio aliye msahau Allah.
Malipo yake naye atatelekezwa na Allah katika mambo yake na shida zake.
Ewe Allah! tujaalie katika watu wenye kutenda mema na utiifu.
“Sema: Hii ndiyo njia yangu, ninalingania kwa Allah kwa kujua, mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Allah! Wala mimi si katika washirikina”. Surat Yusuf: 108.
Hii ndiyo njia yetu, kuwalingania watu katika dini ya Allah kwa kujua(elimu), pamoja na kuthibiti katika haki na ukweli.
Kamwe! Hatuto fuata isipo kuwa yale yanayo ridhiwa na Allah tu.
MAZINGATIO:
Ni wajibu kulingania katika dini ya kweli ya Allah.
“Sema: Hii ndiyo njia yangu, ninalingania kwa Allah kwa kujua, mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Allah! Wala mimi si katika washirikina”. Surat Yusuf: 108.
Kulingania kwetu kwa ajili ya Allah, kumejengwa juu ya misingi ya elimu na imani, kwa kushikamana na tawhidi na kujiepusha na ushirikina.
Ewe Allah! Tujaalie kuwa wenye kufuata njia hii njema.
MAZINGATIO:
Umuhimu wa kushikamana na tawhidi na imani katika kulingania
“Basi mbona hawakuwemo katika watu wa kabla yenu wenye vyeo na wasaa wanao kataza uharibifu katika nchi, isipo kuwa wachache tu, ambao ndio tulio waokoa? Na walio dhulumu walifuata starehe zao,na wakawa ni wakosefu. Wala hakuwa Mola wako Mlezi wa kuihiliki miji kwa dhulma tu na hali watu wake ni watenda mema”. Surat Hud : 116 - 117
Lau katika uma zilizo pita kusingekuwa na watu wanao kataza uovu katika miji, basi wange angamizwa wote, lakini Allah aliwaokoa wachache miongoni mwao ambao walikuwa wakikataza maovu.
“Basi mbona hawakuwemo katika watu wa kabla yenu wenye vyeo na wasaa wanao kataza uharibifu katika nchi, isipo kuwa wachache tu, ambao ndio tulio waokoa? Na walio dhulumu walifuata starehe zao,na wakawa ni wakosefu. Wala hakuwa Mola wako Mlezi wa kuihiliki miji kwa dhulma tu na hali watu wake ni watenda mema”. Surat Hud : 116 - 117
Allah haangamizi miji isipo kuwa pale uovu unapo endelea kufanywa na watu wake.
Lakini watu wake wakiwa wema, huwa anawalinda na kuwahifadhi.
Basi, ni wajibu wetu wote kutengeneza hali zetu na kuwa wema.
“Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa(mfwatizi), wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo yajua”. Surat Al-Baqara: 30.
Allah mtukufu amemchagua Binadamu kuwa ni Khalifa (Kiongozi) katika ardhi, licha ya kuonekana na baadhi ya viumbe kuwa ni muovu.
Lakini ujuzi wa Allah ni mpana sana na sisi hakuna tulijualo katika ujuzi wa Allah ila kwa msaada wake.
“Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa(mfwatizi), wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo yajua”. Surat Al-Baqara: 30.
Malaika walihoji kuhusu ufisadi wa Binadamu, lakini Allah anajua wasiyo yajua.
Basi, tuwe wema katika dunia hii ili kuthibitisha hekima ya Allah ya kutuleta duniani.
“Na lau kama wangeli simama sawasawa juu ya njia tungeli wanywesha maji kwa wingi. Ili tuwajaribu kwa hayo, na anaye puuza kumkumbuka Mola wake Mlezi atamsukuma kwenye adhabu ngumu”.
Surat Al-Jinn: 16 – 17.
Lau kama watu watasimama sawasawa katika njia iliyo nyooka (Uislamu), basi watapata baraka nyingi kutoka kwa Allah, lakini kuacha kumkumbuka Yeye ni sababu ya kupata adhabu.
MAZINGATIO:
Umuhimu wa kusimama sawasawa katika njia sahihi(Uislamu) na kutubu.
“Na lau kama wangeli simama sawasawa juu ya njia tungeli wanywesha maji kwa wingi. Ili tuwajaribu kwa hayo, na anaye puuza kumkumbuka Mola wake Mlezi atamsukuma kwenye adhabu ngumu”.
Surat Al-Jinn: 16 – 17.
Kusimama sawasawa katika dini ya Allah huleta baraka na rehema.
Ama kupuuza utajo wa Allah husababisha kupata adhabu.
Basi, ni wajibu wetu kupupia jambo la kusimama sawasawa katika dini.
MAZINGATIO:
Njia ya kweli na ya mafanikio ni kumkumbuka Allah kwa wingi.
“Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamungu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi. Lakini walikanusha basi tukawaangamiza kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma”. Surat Al-A’raf: 96.
kumchamungu basi baraka za mbinguni na ardhini zitawafungukia, lakini wanapo kanusha haki husababisha kuangamizwa.
MAZINGATIO:
Kushikamana na imani na uchamungu ni sababu ya kupata baraka na mafanikio katika maisha Imani na ucha Mungu huleta baraka kutoka kwa Allah.
“Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamungu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi. Lakini walikanusha basi tukawaangamiza kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma”. Surat Al-A’raf: 96.
Ama kukanusha haki matokeo yake huwa ni kuangamizwa.
Basi, tuwe ni wenye kushikamana na ucha Mungu ili tupate baraka zake.
MAZINGATIO:
Baraka zinapatikana kwa kutubu na kushikamana na uchamungu.
“Hakuna kulazimisha katika Dini. Kwani uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shetani na akamuamini Allah bila ya shaka amekamata kishikio Madhubuti, kisicho vunjika. Na Allah ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua”. Surat Al-Baqara: 256.
Hakuna kulazimisha katika Dini, kwa sababu imani ni jambo huru kwa mwenye kubainikiwa na uwongofu kutokana na upotofu.
Mwenye kuchagua imani ya kumuamini Allah, bila ya shaka ameshika Kamba Madhubuti isiyo katika.
MAZINGATIO:
Uhuru wa kuamini, ndiyo msingi wa kumuamini Allah bila
“Hakuna kulazimisha katika Dini. Kwani uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shetani na akamuamini Allah bila ya shaka amekamata kishikio Madhubuti, kisicho vunjika. Na Allah ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua”. Surat Al-Baqara: 256.
kulazimishwaKufuata Dini ni hiyari ya moyo. Mwenye kuchagua imani ya Allah na kuifuata haki, basi ameshikamana na Kamba Madhubuti.
Ewe Allah! Tujaalie kuwa katika watu wa haki.
MAZINGATIO:
Umuhimu wa kuchagua imani kwa uhuru wa nafsi bila kulazimishwa.
Angeli taka Mola wako Mlezi wangeli amini wote waliomo katika ardhi. Je, wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini? Surat Yunus: 99
Allah anao uwezo wa kuwalazimisha watu wote waliomo ardhini kuamini, lakini amempa kila mtu uhuru wa kuchagua. Na atawahesabu kila mmoja wao siku ya kiama. Kwa hiyo, hakuna sheria ya kulazimisha kuingia katika Dini (japokuwa haki ipo katika umma wa Nabii Muhammad rehma na amani ziwe juu yake).
Allah hawalazimishi watu kuamini, bali amewaacha huru katika kuchagua kwao kati ya haki na batili.