Mtu Mmoja kama Taifa :
Wakati Mtu Mmoja Anaumba
Athari ya Ummah Wote
Katika nyakati ngumu zenye changamoto, watu wakweli hudhihirika, mtu asiye julikana jina lake, lakini mtazamo wake (nia yake njema) ulimuokoa Nabii.
Mtu Mmoja kama Taifa
Lau katika uma zilizo pita kusingekuwa na watu wanao kataza uovu katika miji, basi wange angamizwa wote, lakini Allah aliwaokoa wachache miongoni mwao ambao walikuwa wakikataza maovu.
Ewe Allah! Tujaalie katika wenye kufanya vizuri.
“Na akaja mtu kutoka mwisho wa mji akipiga mbio, akasema: Ewe Musa! Wakubwa wanashauriana kukuuwa. Basi toka! Hakika mimi ni katika wanao kupa nasaha”. Surat Al-Qasas: 20.
Katika nyakati ngumu zenye changamoto, watu wakweli hudhihirika, mtu asiye julikana jina lake, lakini mtazamo wake (nia yake njema) ulimuokoa Nabii.
Nasaha njema katika wakati wake zinaweza kubadilisha hali ya umma.
“Na akaja mtu kutoka mwisho wa mji akipiga mbio, akasema: Ewe Musa! Wakubwa wanashauriana kukuuwa. Basi toka! Hakika mimi ni katika wanao kupa nasaha”. Surat Al-Qasas: 20.
Usisubiri uwe mashuhuri ili kuleta athari.
Inatosha tu kuwa Mkweli, Shujaa, Mwenye utakaso (ikhlas) katika nasaha zako, na hatimaye historia ikaandikwa kwa mtazamo wako na si jina lako.
“Hakika hii Qur’an inaongoa kwenye yaliyo nyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba watapata malipo makubwa”. Surat Al-Israa: 9.
Katika ulimwengu zipo njia nyingi za kufikia mambo. Lakini ipo njia moja tu ya kuleta mafanikio na uongofu, ambayo haina kona kona wala upotofu.
Basi, jitahidi kuitafuta nuru katika Kitabu cha Allah (Qur’an) utapata njia sahihi ya uongofu!
“Hakika hii Qur’an inaongoa kwenye yaliyo nyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba watapata malipo makubwa”. Surat Al-Israa: 9.
Siyo ahadi ya kawaida, bali ni bishara njema ya kweli kutoka kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote, kwa kila Muumini anaye fanya mema kuwa atapata malipo makubwa yanayo msubiri.
Eee, uzuri ulioje wa ahadi hii, na ukarimu ulioje wa Mola wetu Mlezi!
“Je, alie kuwa maiti kisha tukamhuisha, na tukamjaalia nuru inakwenda naye mbele za watu, mfano wake ni kama aliyoko gizani akawa hata hawezi kutoka humo? Kama hivyo makafiri wamepambiwa waliyo kuwa wakiyafanya”. Surat Al-An’aam: 122.
Tambua kuwa kuongoka si kuwa na elimu tu, bali ni maisha mapya yanayo chimbuka kutoka moyoni, na nuru inayo kuangazia njia katikati ya giza la watu!
MAZINGATIO:
Nuru ya imani ndiyo inayo uangazia moyo kutembea na uongofu!
“Je, alie kuwa maiti kisha tukamhuisha, na tukamjaalia nuru inakwenda naye mbele za watu, mfano wake ni kama aliyoko gizani akawa hata hawezi kutoka humo? Kama hivyo makafiri wamepambiwa waliyo kuwa wakiyafanya”. Surat Al-An’aam: 122.
Tofauti iliyopo kati ya anayeishi kwa nuru ya imani na anaye zama katika viza vya maasi, ni kama tofauti iliyopo kati ya mtu aliye hai anaye tembea vizuri kwa kuona kwa macho yake na mtu aliye kufa asiye ona!
Wale walio amini na zikatulia nyoyo zao kwa kumkumbuka Allah. Hakika kwa kumkumbuka Allah ndiyo nyoyo hutulia!
Surat Ar-Ra’d: 28
Tunapo tafuta utulivu katika nyakati za fujo na changamoto, tutaupata katika sehemu moja tu: kipindi cha moyo unapo mkumbuka Mola wake Mlezi kwa ukweli kabisa!
Utulivu haununuliwi, lakini ni zawadi itokanayo na mtu anapo jiegemeza kwa Allah!
“Nikasema: Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi, hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe. Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo.Na atakupeni mali na watoto, na atakupeni mabustani na atakufanyieni mito”. Surat Nuh: 10-12.
Kuomba msamaha si kwa ajili ya kutaka kusamehewa dhambi tu, bali ni mojawapo ya milango ya kupata riziki, na utulivu wa nafsi, na ukunjufu wa vipato.
Yeyote mwenye kupata dhiki ya dunia, basi auelekee mlango mmoja tu wa mbinguni kwa kusema neno moja tu: Naomba msamaha ewe Allah!
“Nikasema: Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi, hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe. Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo.Na atakupeni mali na watoto, na atakupeni mabustani na atakufanyieni mito”. Surat Nuh: 10-12.
Mbingu zinapo kuwa kame, na riziki kuchelewa, na kheri kupungua. Dawa kubwa iliyopo mbele yako ni moja tu: Kuomba msamaha.
Hakika hiyo ni ahadi ya Mola Mlezi ambayo haiendi kinyume, kwani ameahidi kukupa mafanikio.
Basi, anza sasa na uthibiti katika hilo, utapata mafanikio makubwa!
“Na Firauni akasema: Niachieni nimuuwe Musa, naye amwite Mola wake Mlezi! Mimi nachelea asije kukubadilishieni dini yenu, au akatangaza uharibifu katika nchi”. Surat Ghafir: 26.
Waovu daima huogopa mabadiliko, na huivisha haki vazi la upotofu.
Firauni hakuogopa ufisadi, bali aliogopa utawala wake kutoweka kwa sababu ya neno la haki alilo kuja nalo Nabii Musa!
“Na Firauni akasema: Niachieni nimuuwe Musa, naye amwite Mola wake Mlezi! Mimi nachelea asije kukubadilishieni dini yenu, au akatangaza uharibifu katika nchi”. Surat Ghafir: 26.
Wakati inapo onekana kufanya mema ni ufisadi katika macho na mitazamo ya madhalimu, tambua kuwa sauti ya haki imewaumiza, na kwamba wito (Da’awa) wako umeanza kuleta matunda yake.
“Wala msifanye uharibifu katika nchi baada ya kuwa imekwisha tengenezwa. Na muombeni Yeye kwa kuogopa na kwa kutumai. Hakika rehema ya Allah iko karibu na wanao fanya mema”. Surat Al-A’araf: 56.
Kufanya uharibifu katika nchi baada ya kuwa imekwisha tengenezwa ni kosa kubwa sana, kwa sababu huondoa kheri
Basi, tahadhari usiwe katika waharibifu baada ya kujua njia bora ya kutengeneza!
“Wala msifanye uharibifu katika nchi baada ya kuwa imekwisha tengenezwa. Na muombeni Yeye kwa kuogopa na kwa kutumai. Hakika rehema ya Allah iko karibu na wanao fanya mema”. Surat Al-A’araf: 56.
Muombe Mola wako Mlezi kwa moyo wa hofu na tumaini. Mlango wa rehema upo karibu, lakini haufunguliwi ila kwa wenye kufanya mema ambao hufanya mema katika ardhi na hawafanyi uharibifu.
“Wale ambao Malaika huwafisha katika hali njema, wanawaambia: Amani iwe juu yenu! Ingieni Peponi kwa sababu ya yale mliyo kuwa mkiyatenda”. Surat An-Nahl: 32.
Uzuri ulioje ikiwa mwisho ukiwa mwema! Na kupokelewa na Malaika kwa amani, na kufunguliwa mlango wa Peponi kwa yale uliyo yatanguliza katika mema!
Mwisho hufupisha safari, basi jichagulie mwenyewe unavyo penda uwe mwisho wako!
“Wale ambao Malaika huwafisha katika hali njema, wanawaambia: Amani iwe juu yenu! Ingieni Peponi kwa sababu ya yale mliyo kuwa mkiyatenda”. Surat An-Nahl: 32.
Matendo yako ya leo ndiyo neno la makaribisho yako ya kesho!
Basi, pandikiza (fanya) kheri katika maisha yako yote, huenda ukawa muda wako wa kuaga maisha uko karibu sana!