Yeye (Allah) ndiye anaye-kuendesheni bara na baharini, .."
Yeye (Allah) ndiye anaye-kuendesheni bara na baharini, mpaka mnapokuwa kwenye jahazi (mashua) na upepo mzuri ukatembea nao kwa kasi na wakaufurahia, upepo mkali uliijia jahazi hiyo na yakawapiga mawimbi kutoka kila upande, na wakadhani kuwa wamezingirwa, hapo walimuomba Allah wakim-takasia dini (utiifu wakisema kuwa, ewe Mola wetu Mlezi): “Kwa Yakini kabisa, endapo utatuokoa katika haya, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru”
Basi (Allah) alipowaokoa, ghafla wakawa wanafanya uovu katika ardhi bila ya haki. Enyi watu, hakika uasi wenu ni hasara kwenu; ni anasa (fupi) za maisha ya duniani. Kisha kwetu tu ndio marejeo yenu, kwa hiyo tutakuambieni yote mliyokuwa mkiyafanya
407
Video zenye uhusiano
Tazama video nyingine kuhusu mada hiyo hiyo