Enyi watu, hakika
yamekujieni mawaidha
kutoka kwa Mola wenu
Mlezi na ponyo (dawa) ya
(maradhi) yaliyomo vifuani
(mwenu) na muongozo na
rehema kwa Waumini
YUNUS 57
Wakati kifua chako kinapopata dhiki na ukawa hujui ni ipi sababu ya machungu ya dhiki hiyo,yaliyomo ndani yake, basi Qur’an inakuja kukupa suluhisho lake na si kukukaripia.
Bali inakuponya maradhi yote uliyo nayo yasiyo onekana kwa macho wala fikra za kawaida.
Enyi watu, hakika
yamekujieni mawaidha
kutoka kwa Mola wenu
Mlezi na ponyo (dawa) ya
(maradhi) yaliyomo vifuani
(mwenu) na muongozo na
rehema kwa Waumini
YUNUS 57
Qur’an si maneno yanayo somwa tu, bali ni mawaidha yanayozindua, na ponyo inayo maliza matatizo, na rahma inayo ulinda moyo wako kwa njia ya upole.
MAZINGATIO:
Nuru ya Qur’an ni yenye kuangaza katika kila tatizo.
Enyi Watu wa Kitabu, kwa hakika kabisa, amekujieni Mtume wetu (Muhammad)
akikuwekeeni wazi mengi mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu (Taurati na Injili) na
akisamehe mengi. Bila shaka, imekujiieni nuru kutoka kwa Allah na Kitabu
kinachobainisha Kwa (Kitabu) hicho Allah anamuongoza anayefuata radhi zake
katika njia za amani na anawatoa katika viza (na) kuwapeleka kwenye nuru kwa
idhini yake, na anawaongoza kwenye njia iliyonyooka
AL-MAIDA 15 - 16
Katika ulimwengu uliofunikwa na giza, Qur’an inakuja kama nuru isiyo kutelekeza, bali inkujulisha njia yenye usalama na amani.
Enyi Watu wa Kitabu, kwa hakika kabisa, amekujieni Mtume wetu (Muhammad)
akikuwekeeni wazi mengi mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu (Taurati na Injili) na
akisamehe mengi. Bila shaka, imekujiieni nuru kutoka kwa Allah na Kitabu
kinachobainisha Kwa (Kitabu) hicho Allah anamuongoza anayefuata radhi zake
katika njia za amani na anawatoa katika viza (na) kuwapeleka kwenye nuru kwa
idhini yake, na anawaongoza kwenye njia iliyonyooka
AL-MAIDA 15 - 16
Qur’an haikutoi katika giza moja tu, bali inakutoa katika viza vingi na kukufikisha katika nuru moja tu ya uongofu iliyo wazi.
MAZINGATIO:
Qur’an inaongoa kutoka katika giza na kupeleka katika nuru.
Na miongoni mwa watu kuna
wanaofanya washirika badala ya
(kumuamini) Allah (pekee);
wanawapenda kama wampendavyo
Allah. Na walioamini wanampenda
zaidi Allah. Na laiti waliodhulumu
wangejua watakapoiona adhabu
kwamba, nguvu zote ni za Allah, na
kwamba, Allah ni mkali wa
kuadhibu
AL-BAQARAH 165
Moyo unapo jaa mapenzi ya kumpenda Allah, basi vitu vyote huwa vidogo katika mapenzi yake, na mizani ya mapenzi ya kweli husimama ipasavyo.
Na miongoni mwa watu kuna
wanaofanya washirika badala ya
(kumuamini) Allah (pekee);
wanawapenda kama wampendavyo
Allah. Na walioamini wanampenda
zaidi Allah. Na laiti waliodhulumu
wangejua watakapoiona adhabu
kwamba, nguvu zote ni za Allah, na
kwamba, Allah ni mkali wa
kuadhibu
AL-BAQARAH 165
Kumpenda Allah si kwa kudai tu, bali huwa kwa utashi wa moyoni unaobadilisha vipaumbele, na kuupa moyo uhuru wa kutofungamana na mambo yasiyo faa.
Hakika walio amini na wakatenda mema Arrahmani Mwingi wa
Rehema atawajaalia mapenzi
MARYAM 96
Unapompenda Allah kwa dhati ya ukweli, hauhitajiki kufanya kazi ya ushawishi ili ukubaliwe na watu, bali Allah mwenyewe mwingi wa rehema atakupa upendo wake kwa hali usiyo itegemea na kukupa mafanikio makubwa katika maisha.
MAZINGATIO:
Mapenzi ya Allah, Mwingi wa rehema ni makubwa kuliko chochote.
Enyi mlioamini, yeyote ataka-yeritadi
miongoni mwenu kwa kuiacha Dini
yake (ya Uislamu), basi Allah ataleta
watu anaowapenda nao
wanampenda, wanyenyekevu mno
kwa waumini (wenzao) na wenye
nguvu sana mbele ya makafiri,
wanapigania Jihadi katika Njia ya
Allah, na hawaogopi lawama za
mwenye kulaumu. Hizo ni fadhila za
Allah humpa amtakaye. Na Allah ni
Mkunjufu, Mwenye kujua sana
AL-MAIDA 54
Heshima kubwa ya Mwanaadam ni yeye kuwa mwenye kupendeza mbele ya Allah, kabla ya kupendwa na yeye.
Enyi mlioamini, yeyote ataka-yeritadi
miongoni mwenu kwa kuiacha Dini
yake (ya Uislamu), basi Allah ataleta
watu anaowapenda nao
wanampenda, wanyenyekevu mno
kwa waumini (wenzao) na wenye
nguvu sana mbele ya makafiri,
wanapigania Jihadi katika Njia ya
Allah, na hawaogopi lawama za
mwenye kulaumu. Hizo ni fadhila za
Allah humpa amtakaye. Na Allah ni
Mkunjufu, Mwenye kujua sana
AL-MAIDA 54
Allah anapo kupenda, utapata thabati na huto ogopa lawama yoyote, na wala hutoibadilisha haki.
MAZINGATIO:
Kuthibiti kwa imani kunapatikana kwa kumpenda Allah.
Na namna hivi tumekufunulia
Qur'ani kwa amri yetu. Ulikuwa
hujui Kitabu ni nini, wala Imani.
Lakini tumekifanya kuwa ni Nuru
ambayo kwayo tunamwongoa
tumtakaye katika waja wetu. Na
hakika wewe unaongoa kwenye
Njia Iliyo Nyooka
ASH-SHUURAA 52
Qur’an siyo majibu yaliyo andaliwa tu, bali ni nuru inayo ambatana nawe hali ya kuwa nawe unaitafuta.
Na namna hivi tumekufunulia
Qur'ani kwa amri yetu. Ulikuwa
hujui Kitabu ni nini, wala Imani.
Lakini tumekifanya kuwa ni Nuru
ambayo kwayo tunamwongoa
tumtakaye katika waja wetu. Na
hakika wewe unaongoa kwenye
Njia Iliyo Nyooka
ASH-SHUURAA 52
Wakati changamoto zinapo kuzonga,hauhitaji kutaabika, bali unahitaji kupata nuru inayo kuangazia na kukuongoza katika kutatua changamoto hizo.
Alif Lam Raa. Hiki ni Kitabu tulichokiteremsha kwako ili
kwacho uwatowe watu kwenye giza uwapeleke kwenye
muangaza, kwa idhini ya
Mola wao Mlezi,
uwafikishe kwenye Njia
ya Mwenye nguvu,
Msifiwa
IBRAHIM 1
Ujumbe wa Qur’an haubadilishi tu anuani, bali unamuokoa mwanaadam kutokana na ujinga.
Alif Lam Raa. Hiki ni Kitabu tulichokiteremsha kwako ili
kwacho uwatowe watu kwenye giza uwapeleke kwenye
muangaza, kwa idhini ya
Mola wao Mlezi,
uwafikishe kwenye Njia
ya Mwenye nguvu,
Msifiwa
IBRAHIM 1
Qur’an haihamasishi dhuluma, bali inakutoa kwenye giza la dhuluma hatua kwa hatua na kukupeleka katika nuru ya haki na uongofu.
Na siku tutakayomfufua
shahidi (Mtume) katika kila
umma kutoka miongoni mwao
atakayethibitisha (kuwa
aliwafikishia ujumbe wa Allah
wakampinga), na tutakuleta
wewe kuwa shahidi wa (watu)
hawa. Na tumekuteremshia
kitabu kikibainisha kila kitu, na
rehema na bishara kwa
Waislamu
ANNAHLI 89
Hakuna dhiki yoyote inayopatikana katika moyo isipokuwa Qur’an inayo ubainifu wake, au muongozo, au rehema.
Na siku tutakayomfufua
shahidi (Mtume) katika kila
umma kutoka miongoni mwao
atakayethibitisha (kuwa
aliwafikishia ujumbe wa Allah
wakampinga), na tutakuleta
wewe kuwa shahidi wa (watu)
hawa. Na tumekuteremshia
kitabu kikibainisha kila kitu, na
rehema na bishara kwa
Waislamu
ANNAHLI 89
Qur’an haikutelekezi katikati ya njia, bali ina ambatana nawe mpaka mwisho na kukupa utulivu wa kweli.
Hakika, mimi
nimeelekeza uso
wangu kwa (Allah)
aliyeumba mbingu na
ardhi, nikiacha itikadi
zote potofu, na mimi
si miongoni mwa
washirikina
AL-AN'AAM 79
Uongofu unaanza wakati moyo unapo fuata haki kwa dhati, na bila kujali kipindi cha ukamiifu wa ufahamu.
Unapo mchagua Allah kiukweli ina maanisha unakuwa umejipa uhuru wa kutokuwa mtumwa kwa yoyote.
Hakika, mimi
nimeelekeza uso
wangu kwa (Allah)
aliyeumba mbingu na
ardhi, nikiacha itikadi
zote potofu, na mimi
si miongoni mwa
washirikina
AL-AN'AAM 79
Unapo mchagua Allah kiukweli ina maanisha unakuwa umejipa uhuru wa kutokuwa mtumwa kwa yoyote.
Mussa tena akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimeza walivyo vizua Hapo
wachawi walipinduka wakasujudu Wakasema: Tunamuamini Mola Mlezi
wa walimwengu wote
ASH-SHUARAA 45: 47
Muda mfupi tu wa kushikamana na haki, ulibadilisha historia ya wachawi, wakawa ni miongoni mwa waumini wenye kusujudu na kumuabudu Allah.
Mussa tena akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimeza walivyo vizua Hapo
wachawi walipinduka wakasujudu Wakasema: Tunamuamini Mola Mlezi
wa walimwengu wote
ASH-SHUARAA 45: 47
Uongofu unaweza kukufikia kwa ghafla, na ukabadilisha kila kitu baada ya hapo.