Na ungeliwaona wakosefu wanvyo inamisha vichwa vyao mbele ya Mola wao Mlezi, (wakisema): Mola wetu Mlezi! Tumeshaona, na tumeshasikia. Turejeshe tukatende mema, kwani hakika sisi tumekwisha kuwa na yakini sasa
ASSAJDAH12
Uhalisia wa mambo utakapo bainishwa baada ya muda wake kufika, haitobakia kwa mtu ila ni majuto tu
Kumbuka kuwa imani haitomfaa mtu baada ya muda wa kufanya matendo kuisha, fanya haraka kutenda mema kabla hujasema: “Najuta, laiti ninge……”
Na ungeliwaona wakosefu wanvyo inamisha vichwa vyao mbele ya Mola wao Mlezi, (wakisema): Mola wetu Mlezi! Tumeshaona, na tumeshasikia. Turejeshe tukatende mema, kwani hakika sisi tumekwisha kuwa na yakini sasa
ASSAJDAH12
Utafika muda wa kila mtu kuona uhalisia wa mambo kwa uwazi, lakini hapatokuwa na muda wa kutenda mema tena!
Yakini ya kweli ni kuamini mwenyewe kwa hiyari kabla ya kufika muda wa kulazimika kuamini hali ya kuwa imani hiyo haitosaidia chochote.
Na litapulizwa barugumu, mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola wao Mlezi
Watasema: Ole wetu! Nani aliye tufufua kwenye malazi yetu? Haya ndiyo aliyo yaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume
YAASIIN
51-52
Kuna siku itakayo tokea ndani yake mambo ambayo mtu hajawahi kufikiria kuwa yatatokea, kipindi cha watu watakapo fufuliwa kutoka makaburini mwao na kuanza kuuliza: “Nani aliye tufufua?
Kukumbuka nguvu za Allah na uwezo wake katika siku ambayo majuto hayatomfaa mtu, hili ni jambo muhimu sana.
Na litapulizwa barugumu, mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola wao Mlezi
Watasema: Ole wetu! Nani aliye tufufua kwenye malazi yetu? Haya ndiyo aliyo yaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume
YAASIIN
51-52
Allah atawafufua wafu wote kwa wakati mmoja, na ahadi yake ya kweli isiyokwenda kinyume itatubainikia.
Basi, ni muhimu kwa sasa(hapa duniani) tuwe makini kuangalia matendo yetu kabla ya kufikiwa na siku hiyo nzito.
Mpaka yanapo mfikia mmoja wao mauti, husema: Mola wangu Mlezi! Nirudishe
Ili nitende mema sasa badala ya yale niliyo yaacha. Wapi! Hii ni kauli aisemayo yeye tu. Na nyuma yao kipo kizuizi mpaka siku watakapo fufuliwa
ALMUUMINUUN
99-100
Katika kipindi ambacho mtu anafikiwa na kifo, hutamani kurudishwa duniani ili afanye matendo mema, lakini wapi, hakuna tena muda wa kupewa kwa ajili ya tamaa hiyo.
Muda ni wa thamani,usisubiri kutenda mema mpaka kiama kikukute.
MAZINGATIO:
Toba ina muda wake, tumia fursa hiyo haraka kabla ya kuisha.
Mpaka yanapo mfikia mmoja wao mauti, husema: Mola wangu Mlezi! Nirudishe
Ili nitende mema sasa badala ya yale niliyo yaacha. Wapi! Hii ni kauli aisemayo yeye tu. Na nyuma yao kipo kizuizi mpaka siku watakapo fufuliwa
ALMUUMINUUN
99-100
Ni nani atakaye tamani kurudi duniani bila ya kujua mafikio yake ya Akhera?!
Maisha ya dunia ndiyo fursa nzuri ya kutenda, ambayo haina badala.
Matendo yako ya sasa ndiyo yatakuwa kipimo cha mafikio yako katika siku ya ahadi (kiyama).
Na wanapoambiwa msifanye uharibifu ardhini wanasema: Hapana, bali sisi niwafanyaji mazuri
Elewa! Kwa yakini, wao ndio waharibifu hasa na lakini hawatambui
AL-BAQARAH
11-12
Katika kipindi ambacho baadhi ya watu wanadai kuwa wanafanya wema, hali ya kuwa kiuhalisia wao ndiyo wanao fanya uharibifu.
Haya huyajua ukweli wake kwa uwazi wale wenye kuzingatia mambo.
Na wanapoambiwa msifanye uharibifu ardhini wanasema: Hapana, bali sisi niwafanyaji mazuri
Elewa! Kwa yakini, wao ndio waharibifu hasa na lakini hawatambui
AL-BAQARAH
11-12
Usidai kuwa unatengeneza hali ya kuwa unapandikiza uharibifu (ufisadi).
Mwanadamu anatakiwa kufikiria na kupima matendo yake kabla ya kujiridhisha kuwa anayo yafanya ni kheri.
Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa (kiongozi) katika ardhi. Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio yakakupoteza kwenye Njia ya Allah. Hakika wanao ipotea Njia ya Allah wakaiacha, watapata adhabu kali kwasababu ya kusahau kwao Siku ya Hesabu
Kufuata matamanio ya nafsi ni chanzo cha kukuweka mbali na njia sahihi, basi usiyaendekeze matamanio yako yakuongoze kwenye upotofu.
Kumbuka kuwa Akhera kuna hesabu na adhabu, kuwa Mwangalifu!
MAZINGATIO:
Ni muhimu kuwa na tafakuri ya kina kuhusu hatma ya kufuata matamanio.
Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa (kiongozi) katika ardhi. Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio yakakupoteza kwenye Njia ya Allah. Hakika wanao ipotea Njia ya Allah wakaiacha, watapata adhabu kali kwasababu ya kusahau kwao Siku ya Hesabu
Kufuata matamanio ya nafsi inaweza kuwa sababu ya upotofu, basi usiisahau siku ya hesabu (siku ya kiyama).
Ishi maisha yako yote kwa kuafikiana na yale anayo yaridhia Allah, ili ufanikiwe katika dunia na akhera.
Soma uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Sala. Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumtaja Allah ndilo jambo kubwa kabisa. Na Allah anayajua mnayo yatenda
Qur’an na Sala ni miongoni mwa ibada zenye athari kubwa katika maisha yetu.
Ibada hizo mbili ni taa inayo angaza njia.
Na sala ni ibada maalumu ambayo inatukataza tusifanye uchafu na maovu.
Na ibada ya dhikri (kumkumbuka na kumtaja Allah) inaufanya moyo kuwa na utukufu na kuufungamanisha na Allah daima.
MAZINGATIO:
Dhikri na Sala ni miongoni mwa ibada zinazo mfikisha mtu kwenye uchamungu.
Soma uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Sala. Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumtaja Allah ndilo jambo kubwa kabisa. Na Allah anayajua mnayo yatenda
Sala si kwamba ni ibada tu bali ni ngao inayo tulinda na kuingia katika maasi.
Basi, kuwa mwingi wa kumkumbuka na kumtaja sana Allah ili upate nguvu ya kiimani na utashi wa kweli.
Kwa hakika kabisa, katika simulizi zao (hao Mitume) kuna mazingatio kwa wenye akili. Haikuwa (hii Qur’an ni) maneno yanayozushwa lakini ni usadikisho (uthibitisho) wa (maandiko matakatifu) yaliyokuwepo kabla yake (Taurati na Injili) na ni ufafanuzi wa kila kitu na ni muongozo na rehema kwa watu wanaoamini
Katika visa vya Mitume kuna mazingatio makubwa kwetu sisi wote.
Ndani yake kuna ukumbusho wa kuzingatia na mafundisho kwa yaliyo tokea kwa wale walio tangulia.
Qur’an siyo kitabu cha mazungumzo tu, bali ni kitabu cha ukweli, muongozo na rehma.
MAZINGATIO:
Ni muhimu kuwa na mazingatio katika visa vya wale walio tutangulia.
Kwa hakika kabisa, katika simulizi zao (hao Mitume) kuna mazingatio kwa wenye akili. Haikuwa (hii Qur’an ni) maneno yanayozushwa lakini ni usadikisho (uthibitisho) wa (maandiko matakatifu) yaliyokuwepo kabla yake (Taurati na Injili) na ni ufafanuzi wa kila kitu na ni muongozo na rehema kwa watu wanaoamini
Kila kisa katika Qur’an kimebeba masomo kwetu ya kweli katika maisha.
Kwa kila mwenye kumuamini Allah atapata kwenye kila Aya muongozo na rehma.
Basi kila mmoja tulimtesa kwa mujibu wa makosa yake. Kati yao wapotulio wapelekea kimbunga cha changarawe; na kati yao wapo walio nyakuliwa na ukelele; na kati yao wapo ambao tulio wadidimiza katika ardhi; na kati yao wapo tulio wazamisha. Wala Allah hakuwa mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wenyewe wakijidhulumu nafsi zao
Kila nafsi itavuna ilicho chuma.
Na mateso ya duniani ni matokeo ya dhulma za mwanaadam kujidhulumu mwenyewe.
Allah hamdhulumu yeyote, lakini watu ndiyo wanaojidhulumu wenyewe.
Basi kila mmoja tulimtesa kwa mujibu wa makosa yake. Kati yao wapotulio wapelekea kimbunga cha changarawe; na kati yao wapo walio nyakuliwa na ukelele; na kati yao wapo ambao tulio wadidimiza katika ardhi; na kati yao wapo tulio wazamisha. Wala Allah hakuwa mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wenyewe wakijidhulumu nafsi zao
Malipo huwa ni kutokana na matendo.
Chochote unacho tenda utavuna.
Zingatia hatima ya kila aliye ipuuza haki ilikuwaje na jifunze kwa walio kutangulia.
Na yote haya tunakusimulia miongoni mwa habari za Mitume yale yanayoupa nguvu moyo wako. Na katika haya imekujia haki na mawaidha na ukumbusho kwa waumini
Visa vya Mitume siyo hekaya tu bali ni masomo yanayo uthibitisha moyo na kuuangazia njia sahihi.
Haki na mawaidha yanayo patikana katika kila kisa ni ukumbusho kwa Waumini.
MAZINGATIO:
Inathibiti ya imani inapatikana kwa kuzingatia visa vya Qur’an.
Na yote haya tunakusimulia miongoni mwa habari za Mitume yale yanayoupa nguvu moyo wako. Na katika haya imekujia haki na mawaidha na ukumbusho kwa waumini
Katika kila habari miongoni mwa habari za mitume tunapata mambo yanayo thibitisha imani zetu na uongofu wa nyoyo.
Qur’an ni ukumbusho na nuru kwa waumini wa kila zama.
MAZINGATIO:
Haki ya wazi inapatikana ndani ya masomo ya Qur’an.