Kuwafanya makafiri kuwa marafiki si katika mahusiano na kuamiliana tu, bali ni kule kuwapenda na kuwanusuru kwa kuwatanguliza dhidi ya dini ya Allah.
Qur’an inatufundisha kuwa mapenzi ya kweli huwa kwa ajili ya Allah tu na kuwapenda waumini. Na kwamba Allah anajua yaliyo fichwa na nyoyo na yanayo tangazwa na ndimi, hakuna linalo fichikana mbele ya Allah kwa mapenzi ya kweli au uongo wake.